Bukobawadau

ASERI KATANGA AITEMBELEA SHULE YA JOSIAH GIRLS NA KUAHIDI MAKUBWA

Ndugu Aseri Katanga katika picha ya pamoja na Wanafunzi na Viongozi wa Shule ya Wasichana ya Josia,Ndugu Aseri ameitembelea shule hiyo na kuahidi kusaidia masuala mbalimbali yanayohusu mifumo ya kompyuta mawasiliano na TEHAMA kwa ujumla.

Ndugu Aseri kwa muda mrefu amekuwa akisaidia Jamii kwa kiasi kikubwa na watoto mashuleni katika nchi wanachama wa Jumuiya ya madola .

Ndugu Aseri akibadilishana mawazo na wanafunzi wa Shule ya Wasichana Josiah iliyopo Manispaa Bukoba.
Ushauri  wa Ndugu Aseri Katanga  kwa diaspora

Mwanadiaspora huyu anasema Tanzania inaweza kupiga maendeleo ya kasi zaidi ikiwa kila mtu atatoa mchango wa mawazo na maono sahihi yakakubalika mpaka ngazi ya juu.

Katanga anasema wapo wana diaspora wengi walio tayari kuchangia nchi endapo vikwazo vitaondolewa. “Diaspora wanataka uraia pacha na si special status (hadhi maalumu) kwa sababu diaspora hawataki kuwa zaidi ya wengine.”

“Wanataka na watoto wao waliozaliwa nje ya nchi nao waje nyumbani wachangie kuleta maendeleo. Hawa vijana wa siku hizi wamesoma kwenye vyuo vikuu vizuri sana, wakipata mwongozo mzuri ni faida kwa nchi ya Tanzania.”
Ndugu Katanga Anasisitiza kuwa diaspora wengi ni wazalendo, wanatuma fedha nyingi nyumbani kusomesha ndugu na jamaa na wanashiriki kazi nyingi za kujitolea kwenye maeneo waliyotoka.

Anasema wanadiaspora wanazungumza na marafiki au wafanyakazi wenzao waje kutembelea Tanzania. Wanajenga nyumba au kulima mashamba hatua inayosaidia kuongeza ajira na mzunguko wa fedha.

Katika makala iliyowahi kuchapishwa katika gazeti la Daily News juu ya Mtanzania huyu, mwandishi Dav Kyungu anamtaja Katanga kuwa ni mfano wa kuigwa kwa makubwa aliyofanyia jamii yake na kumfanya Malkia Elizabeth kumtuza.





 

Next Post Previous Post
Bukobawadau