Bukobawadau

ALMUNI WA KIBETA SHULE YA MSINGI WAIKUMBUKA SHULE

Umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma Shule ya Msingi Kibeta (zamani ikijurikana kama Kishasha Extended Primary School) Wametoa mchango wa Madawati na Viti vya waalimu waliopo shuleni hapo kwa sasa na kuwaasa wadau wa maendeleo ya elimu popote walipo  na wazawa wa Kata ya Kibeta na maeneo jirani kuunga juhudi hizi  ikiwa ni katika kuunga mkono  juhudi za Serikali kwenye sekta ya elimu.

Picha ya pamoja Almuni wa Shule ya Kibeta,Walimu na wanafunzi pamoja na Uongozi wa Serikali wa Kata ya Kibeta.

Mmoja wa alumni na mdau wa Maendeleo Eng.. Bennie Muberwa Mushumbusi akitoa maelezo na madhumuni hasa ya kusaidia shule hiyo iliyopo Kata ya Kibeta ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba.

Akizungumza kwa niaba ya Wenzake Eng. Mushumbusi amesema wametoa Jumla ya madawati 24 na Viti vya walimu 12 kwa ajili ya kumpunguza changamoto zilizopo shuleni hapo, amesema michango ya fedha za kununua Madawati hayo imetoka kwa Almuni wa shule hiyo na baadhi ya marafiki zake wapenda maendeleo.

"Sisi Almuni hatupendezwi na mazingira pamoja huaba na changamoto tulizoziona kwenye shule yetu. Nilifika kuwatembelea mkanieleza changamoto mbalimbali nami nikiwashirikisha wenzangu na sasa tumeanza kupunguza kidogo kidogo tatizo likiwemo hili la Madawati na Viti vya ofisi za Waalimu, na tunatalaji kuwa  michango itaendelea .

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kibeta Mwl.Geofrey Lutalala pichani kushoto akitoa maelezo kwa Almuni waliotembelea shule hiyo ,katikati ni Bi Victoria Rweikiza aliyetoka Norway na Eng. Mushumbusi.

Mwalimu Mkuu ameeleza changamoto mbalimbali ikiwemo pia uhitaji wa Photocopy mashine kwa ajili ya kuzalisha mitihani ya majaribio shuleni hapo.

Mwl.Geofrey Lutalala amabye ni mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kibeta anasema licha ya kuwepo changamoto pia anawashutumu wazazi wa wanafunzi katika shule hiyo kwa kushindwa kuonyesha ushirikiano na walimu wa shule hiyo hususani katika kutekeleza wajibu wao kama wazazi katika maendeleo ya Wanafunzi pamoja na Shule kwa Ujumla akitolea mfano suala la wazazi kutofuastilia maendeleo ya wanafunzi wawapo shuleni.

Muonekano wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta wakiwa Darasani
Eng. Mushumbusi pamoja na Fundi Seremara wakiwakirisha madawati kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kibeta

 

Ugeni ukikagua mazingira kujionea hali ya miundombinu kama unavojionea kupitia picha...
Picha ya Juu ikionyesha mazingira halisi ya Shule ya Msingi Kibeta iliyopo Manispaa ya Bukoba

Muendelezo wa matukio ya picha Shule ya Msingi Kibeta
Mwl.Geofrey Lutalala katikati akiwa na Wazazi wa Binti Neema aliyafanya matokeo ya Darasa la Saba katika Somo la hesabati ambapo kwa juhudi za Almun itayari binti huo amepata ufadhili wa kusoma  katika shule bora za Babro Johnson inazoziendesha na Prof. Anna Tibaijuka
Baadi ya Viti vilivyokabidhiwa ambapo zoezi la ukusanyaji michango bado linaendelea
"Mmoja wa Alumni Eng Bennie Mushumbusi akisaini kitanu cha wageni mara baada ya kuwasirishaa mchango wa viti na madawati kwa shule ya Msingi Kiteta iliyopo Manispaa ya Bukoba.

Afisa Elimu Kata Kibeta ,Themistocles Mutasingwa akisalimiana na Eng Bennie Mushumbusi mdau mkubwa wa maendeleo
 

Pichani kushoto ni Afisa Elimu Kata Kibeta ,Themistocles Mutasingwa akiwa ameambatana na viongozi wengine wa kata kibeta katika tukio hili la kukabidhi Viti na Madawati kutoka kwa Almuni waliosoma Shule ya Msingi Kibeta

Taswira mbalimbali pichani.


Baadhi ya madawati ambayo yametolewa na mdau Eng. Grayson Bankobeza wa Houston, Taxas, USA
Madawati yaliyotolewa kama msaada kwa Shule ya Msingi Kibeta
Muonekano wa baadhi ya Viti vilivyokabidhiwa shuleni hapo kutoka kwa Almuni

Next Post Previous Post
Bukobawadau