Bukobawadau

POSTA KAGERA WAKABIDHI KOMPYUTA 5 MUBUKA SEKONDARI KWA MH. DKT KIKOYO

Mbunge wa Jimbo la Muleba kusini Dkt. Oscar Kikoyo akabidhi Kompyuta Tano Katika Shule ya Sekondari Mubuka iliyopo Kata ya Mubunda Wilayani Muleba Mkoani Kagera kwa lengo la kuinua kiwango Cha taluuma kwa wanafunzi nakuinua kiwango cha utendaji na uwezo wa kufanya kazi kwa walimu.
Akikabidhi kompyuta hizo Dkt. kikoyo amesema kuwa kompyuta hizo zimetolewa na Serikali na kusafirisha na Shirika la Postal nchini ambapo amewawataka Walimu wa shule hiyo kuzitumia kwa malengo yaliyopangwa ili ziweze kuleta tija kwa wanafunzi.
Katika makadhiano hayo ya computer, Kaimu Meneja wa Mkoa wa Shirika la Posta Ndugu Antidius Rukwatage pichani ambao ndio wasafirishaji walipewa nafasi ya kuelezea huduma zao.
...
Kaimu Meneja wa Mkoa alielezea huduma za Posta kama ifuatavyo:
Usafirishaji wa barua na vifurushi Kwa njia ya kawaida na usafirishaji wa barua na vifurushi Kwa njia ya haraka (EMS).
Kwa kusafirisha vifurushi Kwa njia ya haraka, Shirika limepata nafasi ya kuaminiwa na Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya habari kusafirisha computer5, ups5,printer, projector za Mubuka Sekondari ambazo amekabidhi Mbunge wa Muleba Kusaini Mhe Dr. Oscar Kikoyo tarehe 23/7/2023
Mbunge wa Jimbo la Muleba kusini Dkt. Oscar Kikoyo akipokea karatasi yenye horodha ya vitu computer5, ups5,printer, projector kwa ajili ya shule ya Sekondari Mubuka ktoka kwa Kaimu Meneja wa Mkoa wa Shirika la Posta Ndugu Antidius Rukwatage
Wadau mbalimbali waliohudhuria na kushuhudia makabidhiano wa vifaa hivyo vya teknologia.
Muonekano wa Bango na baadhi ya Majengo ya Shule ya Sekondari Mubuka
Baadhi ya Walimu wa  Shule ya Sekondari Mubuka iliyopo Kata ya Mubunda Wilayani Muleba.
Pia tarehe 20/7/2023, katika Jimbo la Bukoba mjini Kwa Mhe Byabato, Shirika la Posta kama lilivyopokea vifaa hivi kutoka Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya habari kupitia UCSAF lilikabidhi computer Tano Tano, ups tanotano, projector na printer Kwa shule za Rugambwa Sekondari,. omumwani na Nshambya Sekondari.
Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato Mbunge Jimbo la Bukoba Mjini, na Naibu Waziri Wa Nishati pichani
Muonekano wa Majengo ya Shule ya Sekondari Rugambwa

Shule nyingine ambazo Shirika la Posta limesafirisha computer kutoka Wizarani kupitia UCSAF ni Rugu Sekondary(Karagwe), Lukoye (Misenyi) na Kagango (Biharamulo)

Kaimu Meneja wa Posta alielezea huduma nyingine za Shirika la Posta kuwa ni Uwakala wa fedha, Duka mtandao, internet cafe na kukodisha majengo
Kaimu Meneja alielezea jinsi Duka mtandao linavyofanya kazi kuwa, wajasiliamali wanaandikisha maduka yao kwenye Duka mtandao la Posta Bure. Baada ya kuandikisha wanapewa nafasi ya kutangaza Biashara zao kwenye Duka letu Bure. Mteja anapopatikana Posta inawasiliana na mjasiliamali na kuuza bidhaa alizochagua mteja.Duka la Posta linampa nafasi mteja kununua bidhaa muda wowote, kutembelea maduka kadhaa bila kuzunguka na kulinganisha bei muda wowote.

Pia Kaimu Meneja wa Mkoa alielezea huduma za kidigitali zinazopatikana ndani ya Posta kuwa ni Duka mtandao (e.shop), Sanduku la Posta kidigitali ambao namba ya simu ndio Sanduku lako la Posta, kufuatilia barua Kwa mtandao wa Posta (track and trace), mfumo wa kutuma na kupokea barua wa Posta Kiganjani na mifumo ya kufuatilia barua ya kimataifa ya CDS na IPS.

Mwisho.


 

 Next Post Previous Post
Bukobawadau