Bukobawadau

MAELFU WASHIRIKI MAZISHI YA ENG.GEORGE MUTABUZI KIJIJINI NSHUNJU


Maelfu ya waombolezaji wameungana na wanafamilia katika Adhimisho la Misa takatifu ya kumuaga na kumuombea Mhandisi George Mutabuzi, aliyekuwa mdau mkubwa wa maendeleo, Mwanakwaya na muwezeshaji wa Kwaya Katoliki Tanzania.
Misa takatifu inaadhinishwa na Padre Hilarius Kamanzi, Padre Chaplain wa Masista Nyaigando Jimboni Bukoba, Nyumbani kwao Mhandisi George Mutabuzi Nshunju Parokia ya Ishozi Jimbo Katoliki la Bukoba.
Awali mwili wa Eng Mutabuzi ulipokelewa na kuombewa na Mhashamu Askofu Msaidizi Method Kilaini, Msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki la Bukoba
Sehemu ya Wanafamilia wakiwa ndani.muda mchache kabla ya Misa takatifu ya mazishi ya mpendwa wetu...
Muonekano wa Jeneza lenye Mwili wa mpendwa wetu.Ndugu Denes akitoa muongozo na taratibu kwa mujibu wa ratiba ya Mazishi ya mpendwa wetu Eng George Mutabuzi.
Endelea kuwa nasi mpaka mwisho kwa mtiriko mzima wa matukio ya picha.
Wanakwaya wa Kanisa kuu wakiendelea kuwajibika kwa nyimbo za kuabudu na kumsifu bwana
Taswira mbalimbali kupitia bukobawadau ,Mazishi ya Eng.George Mutabuzi
Taratibu za kutoa salaam za rambirambi zikiendelea....
Salaam za rambirambi kutoka kwa mwakilishi wa Kapotive Star Singers.
Mama Victar akiwakilisha Salaam za rambirambi kwa niaba ya Wanachama wa Bokoba Woman Group.
Bwana Jamal Kaluma na Mtaalam Peter Dk wakitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Wanachama wa  Yanga Tawi la Bukoba.
Jamal Kalumna msemaji wa Yanga Tawi la Kagera
Utaratibu wa kutoa salaam za rambirambi ukiendelea kwa kuzingatia makundi mbalimbali.
Mr &Mrs Claudi Mutabuzi wakiteta wakati taratibu nyingine zikiwa zinaendelea.
Makundi mbalimbali yakendelea kutoa salaam za rambirambi

Misa takatifu ikiendelea kuadhimishwa  na Padre Hilarius Kamanzi, Padre Chaplain wa Masista Nyaigando Jimboni Bukoba, Nyumbani kwao Mhandisi George Mutabuzi Nshunju Parokia ya Ishozi Jimbo Katoliki la Bukoba.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa safari ya mwisho maisha ya mpendwa wetu Eng.George Mutabuzi
Mapadre wakiendelea kuongoza Misa ya kumuombea mpendwa wetu Eng.George Mutabuzi
Muendelezo wa matukio ya picha kutoka msibani hapo.
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiwa unaendelea

Uncle Majid Kichwabuta akitoa heshima zake za mwisho kuaga Mwili wa mpendwa wetu Eng.George Mutabuzi
Al hajji Yahya Kajuna wakati wa kutoa heshima zake za mwisho kwa rafiki yake mkubwa Eng.George Mutabuzi
Umati wa watu katiba misa ya kumuaga mpendwa wao Eng.George Mutabuzi
Simanzi,Vilio na machozi vikitawala kwa waombolezaji wakati wa kutoa heshima za mwisho Mwili wa Eng.George Mutabuzi
Watoto wa kuzaliwa na mpendwa wetu Eng.George Mutabuzi wakitoa heshima za mwisho
Pole sana ndugu Claudi Mutabuzi kwa kumpoteza Kaka yako


Watoto wa Marehemu Eng.George Mutabuzi wakikabidhi  vifaa mbalimbali kwa Padre wa Parokia ya Ishozi kama ishara ya kuendeleza yale yote aliyokuwa akiyafanya Baba yao mpendwa
Muonekano wa Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu George Mutabuzi
Muendelezo wa matukio ya picha...

Umetangulia EngGeorge Mutabuzi,Nenda Salama Kaka,Hakika umehakikisha hadithi na simulizi  ya maisha yako inakuwa na mwisho mzuri
Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu George Mutabuzi likiingizwa kaburini.
Muendelezo wa matukio ya picha...
Umetangulia EngGeorge Mutabuzi,Nenda Salama Kaka,Hakika umehakikisha hadithi na simulizi  ya maisha yako inakuwa na mwisho mzuri
Zoezi la kuweka mashada ya maua likiwa linaendelea..
Watoto wakiwa tayari kuweka shada la maua
Mama mjane wa Mpendwa wetu Eng.George Mutabuzi akiweka shada katika kwenye kaburi la mme wake.

Mwanzo wa matukio ya picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu mara baada ya mazishi.
Wajukuu na Watoto wa familia katika picha ya pamoja katika kaburi la mpendwa wao Eng George Mutabuzi.
Endelea kufuatilia kurasa zetu za facebook na Instagram kwa matukio ya papohapo #Bukobawadau.
..........
Next Post Previous Post
Bukobawadau