Bukobawadau

POSTA KAGERA WAFANYA KIKAO KAZI KUKUMBUSHANA MALENGO 2023/24

BUKOBA:Tarehe 8/8/2023 Wafanyakazi wote wa Shirika la Posta Mkoa wa Kagera walikuwa na kikao kazi. Wafanyakazi waliohudhuria ni kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Kagera ikiwa ni Bukoba, Karagwe, Misenyi, Biharamulo, Ngara na Muleba.

Mwenyekiti wa kikao ambaye ndiye Meneja wa Mkoa ndugu Joseph Mutatina alieleza madhumuni ya kikao kuwa ni kama ifuatavyo:
1. Kupata uelewa wa pamoja wa wafanyakazi wa Posta juu ya malengo na mipango ya Shirika Kwa mwaka wa fedha 2023/24
2.Kupata taarifa ya utendaji kazi Kwa mwaka wa fedha 2022/23
3. Kujadili na kuelewa pamoja upimo wa utendaji kazi Kwa Kila mfanyakazi
4. Kuweka mikakati ya kuongeza mapato ya pamoja na Kila wilaya moja moja.
5. Kuwa na uelewa wa pamoja juu ya Mpango Mkakati wa 8 wa Shirika wa Mwaka 2022- 2026 ambao unasisitiza ukuaji wa Biashara Kwa kutumia Posta ya kidigitali.

Kikao kilianza Kwa sala ya Shirika iliyofuatiwa na mada ya Afya ya akili iliyotolewa na mtoa mada ndugu Issa Mrimi kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Ndugu Issa Mrimi alisisitiza kuepuka msongo wa mawazo.alieleza kuwa ukiwa na msongo wa mawazo huwezi kutimiza majukumu yako ipasavyo yakiwa Niya kifamilia na kiofisi vilevile. Alieleza jinsi ya kuepuka msongo wa mawazo na jinsi kumsaidia mtu mwenye msongo Kwa kutoa msaada wa awali na inaposhindikana kumpa rufaa.

Katika kikao kazi hicho Meneja wa Mkoa Ndugu Joseph Mutatina, alisisitiza Kila mtumishi wa Posta kuwa na uelewa wa huduma zote za Posta.Pia alisisitiza Kila mtumishi kuwa balozi mzuri wa Posta ili kuinua kismati Cha Shirika.

Huduma za Shirika la Posta ni pamoja na kusafirisha barua na vifurushi Kwa njia ya haraka, kusafirisha barua na vifurushi Kwa Kwa njia ya kawaida, huduma za Uwakala wa mabenki, mitandao ya simu, bima na kuuza tiketi za ndege, huduma ya kusafirisha sampuli za binadamu, huduma za internet, Duka mtandao na huduma za kukodisha majengo.

Meneja wa Mkoa alisisitiza watumishi kutumia huduma za kidigitali zinazotolewa na Shirika la Posta. Aliwaekeza watumishi kuwa Posta inapatikana kwenye mitandao ya Twitter, Instagram, Facebook na linked. Meneja alisisitiza kuwa mfumo wetu wa Posta Kiganjani unazidi kuboreshwa na kumpa urahisi mtumiaji.

Meneja wa Mkoa Ndugu Joseph Mutatina (wa pili Toka kulia waliokaa) na kushoto kwake ni msimamizi huduma za Ndugu Antidius Rukwatage.kulia kwake (mwenye Tshirt ya blue) ni mtoa ndugu Issa Mrimi kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa na anayefata ni Mhasibu wa Mkoa Ndugu Patrick Mwakasege. Waliosimama ni Postamasta wa ofisi za Posta zilizopo wilayani. Kutoka kulia ni Postamasta wa Kyaka, Ngara, Kamachumu, biharamulo na Muleba

Pichani wanaonekana wajumbe wakati wanasikilizasalamu za Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo Kwa watumishi wote zilizorushwa Moja Kwa Moja kidigitali na kusikilizwa kwenye TV inayonasa mawimbi ya computer bila kutumia waya(wireless)
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Kagera wakati Kikao kazi kiiendelea
Katika Picha ya pamoja baada ya wajumbe kusikiliza salamu za Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo Kwa watumishi wote zilizorushwa Moja Kwa Moja kidigitali na kusikilizwa kwenye TV inayonasa mawimbi ya computer bila kutumia waya(wireless).

Picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mkutano wa Bukoba Coop hote
Wafanyakazi  wote wa Shirika la Posta Mkoa wa Kagera katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mkutano wa Bukoba Coop hotel mara baada ya kikao Kazi kilichofanyika tarehe 8/8/2023.Next Post Previous Post
Bukobawadau