Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awaandalia hafla ya Chakula cha mchana Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani ambao wanatoa huduma katika Hospitali ya Selian Lutheran iliyopo Mkoani Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Madaktari Bingwa wa Mifupa
kutoka California nchini Marekani pamoja na wageni mbalimbali Ikulu Chamwino
Mkoani Dodoma tarehe 13 Agosti, 2023. Mhe. Rais Samia aliwaandalia Madaktari hao
wanaotoa huduma ya upasuaji katika Hospitali ya Selian Lutheran Mkoani Arusha Chakula
cha mchana kuwashukuru kwa moyo wao wa kujitolea kuwasaidia Watanzania katika
sekta hiyo ya Afya
Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani, Tanzania pamoja na wageni wengine wakiwa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kwa ajili ya hafla ya Chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwashukuru kutokana na mchango wao kwa jamii tarehe 13 Agosti, 2023.Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani, Tanzania pamoja na wageni wengine wakiwa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kwa ajili ya hafla ya Chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwashukuru kutokana na mchango wao kwa jamii tarehe 13 Agosti, 2023.
Viongozi mbalimbali wa Serikali
waliohudhuria hafla ya Chakula cha mchana kwa ajili ya kuwashukuru na
kuwapongeza Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani pamoja
na wale wa Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe
13 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,
viongozi wengine wa Serikali kwenye picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa
Mifupa kutoka California nchini Marekani pamoja na wale wa Tanzania, Ikulu
Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Agosti, 2023.