Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan afungua Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika, Jijini Dodoma
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta
utepe pamoja na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central
Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani kuashiria ufunguzi Rasmi wa
Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye Sherehe
zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini
Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023. Engine katika picha ni Mkuu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania Mhashamu Dkt. Maimbo Mndolwa pamoja na Maaskofu
wengine wa Kanisa hilo nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Muonekano wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika ambalo limefunguliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu tarehe 15 Agosti, 2023.Muonekano wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika ambalo limefunguliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu tarehe 15 Agosti, 2023.