Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Dkt. Dorothy Gwajima akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao cha
kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kilichofanyika Agosti 22, 2023 jijini
Dodoma.Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalum Dkt. John Jingu akiwasilisha utekelezaji wa majukumu ya Idara ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao kilichofanyika Agosti 22,
2023 jijini Dodoma
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Vickness Mayao akifafanua
baadhi ya mambo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara yake mbele ya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa
kikao kilichofanyika Agosti 22, 2023 ,jijini Dodoma.Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya
Jamii Mhe. Mariam Kisangi akitoa maelekezo, maoni na ushauri kwa Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakati
ilipokuwa ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kilichofanyika Agosti 22,
2023 ,jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo
ya Jamii wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kilichofanyika Agosti 22,
2023 ,jijini Dodoma.Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakiwa katika kikao cha Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati Wizara
ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kilichofanyika Agosti 22, 2023 ,jijini
Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
Na WMJJWM Dodoma
Serikali
imesema uanzishaji wa Mfumo wa ramani ya utambuzi wa Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali itasaidia kutatua changamoto za upatikanaji wa taarifa
muhimu kwa Umma kuhusu Mashirika hayo.
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Dkt
Dorothy Gwajima ameyasema hayo wakati akijibu hoja mbalimbali za Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa
kikao na Kamati hiyo Agosti 22, 2023 jijini Dodoma.
Waziri
Dkt. Gwajima amesema Mfumo huo utawezesha wananchi na wadau kufuatilia
na kujua namna Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanavyofanya kazi ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali katika maeneo yao na kwa namna gani
wanaweza kupata fursa ya kunufainika na miradi hiyo.
"Nimeunda
kikosi kazi maalum kwa ajili ya kuratibu na kuzileta NGOs pamoja kwenye
majadiliano ya jinsi gani kuimarisha uelewa wa jamii kwenye utekelezaji
wa shughuli za maendeleo ambapo pia Wahe. Wabunge watapata fursa ya
kujenga uelewa kwa upana zaidi" amesema Dkt. Gwajima.
Awali
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu amesema Wizara kwa mwaka huu
imesajili na kuratibu jumla ya Mashirika 9687, kati yao Mashirika ya
kimataifa ni 578, Mashirika ya Kitaifa 8001, Mashirika ya kimkoa 464 na
Mashirika ya kiwilaya 647. Mashirika hayo yanatekeleza afua mbalimbali
katika maeneo tofauti nchini.
Dkt.
Jingu ameongeza kuwa Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa NGOs inafanya
mafunzo mbalimbali kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuwapa elimu
hiyo kwa kufuata taratibu na Sheria zilizopo.
Wizara
kwa kushirikiana na Wasajili wasaidizi katika Mikoa na Halmashauri
nchini wamefuatilia jumla ya Mashirika 2663 ambayo ni zaidi ya asilimia
100 ya Mashirika yaliyopanga kufikiwa.
Akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya masuala kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi
na Maendeleo ya Jamii Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali,
Vickness Mayao amesema mfumo wa ramani ya kidigitali utatambua afua
mbalimbali zinazofanywa na Mashirika yaliyopo nchini ili kurahisisha
upatikanaji wa taarifa za Mashirika yaliyopo na afua zinazotekelezwa.
Ameongeza
kuwa suala la msamaha wa Kodi kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni
ajenda ambayo imeibuka katika Majukwaa ya NGOs yanayoendelea kufanyika
kwenye ngazi ya Mikoa ila Serikali imeendelea kutoa elimu kwa wadau kwa
mikoa kupitia Kitabu cha Mwongozo wa kuomba msaada wa Kodi kwa Mashirika
hayo.
Naye Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii
Mhe. Mariam Kisangi ameipongeza Wizara kwa utaratibu mzuri wa uratibu
wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwani kuna utofauti Mkubwa
kabla ya Sheria ya NGOs kuboreshwa .
"Ukitaka
kujipima umefika wapi na kama umefanikiwa angalia tulipotoka hapo
mwanzo katika masuala ya usajili na uratibu wa NGOs na sasa naona mifumo
imeboreshwa sana na hasa tulipoingia katika mifumo ya kidigitali"
alisema Mhe. Mariam
MWISHO