Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira Amezindua kampeni
za CCM katika jimbo la Musoma mjini lenye kata 16 ambapo kata mbili
kati ya hizo wagombea udiwani wa chama hicho wamekosa wapinzani.
Ndg.
Wasira amewataka watu wanaohoji kwanini wanamsifia Mwenyekiti wa chama
hicho Samia Suluhu Hassan kuacha kulalamika badala yake nao wafanye
mambo mazuri ya maendeleo ili wasifiwe.
Amesema
katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake Rais Samia amefanya
mambo makubwa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma
za kijamii ikiwemo katika sekta za afya,maji,elimu na sekta zingineElimu na sekta zingine na
kwamba chama chake bado kinalenga kufanya mambo mengine makubwa kwa
wananchi.
Akizungumza
mjini Musoma leo Septemba 6,2025 kwenye uzinduzi wa kampeni za chama
hicho katika jimbo la Musoma Mjini, Wasira amesema lengo la chama hicho
ni kuendelea kushika dola ili kuwatumikia wananchi na ndio maana
wameandaa ilani bora yenye kujibu mahitaji na changamoto zete za
wananchi.
"Sasa
wanalalmika nini wakati hawana chochote walichokifanya,sisi lazima
tumasifie wa kwetu kwasababu amefanya mengi sana na tunayaona,sasa wewe
unalalamika wakati hata zahanati haujajenga,fanya maendeleo na wewe
usifiwe kwasasa tuko na mama Samia," amesema.
Wasira
amesema chama hicho kina malengo mazuri na wananchi na ndio maana
kimerudi tena kuomba ridhaa ya kushika dola huku akisema katika jimbo la
Musoma mjini na mkoa mzima wa Mara yapo mengi mazuri yaliyopangwa
kufanyika kwa maslahi ya wakazi wa jimbo hilo.
Amesema
miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kufanywa na chama hicho katika Mkoa
wa Mara kwa ujumla ni pamoja ujenzi wa vituo vya afya vipya 18, zahanati
mpya 37 pamoja na huku sekta ya elimu na zingine zikitarajiwa kufanyiwa
maboresho makubwa.
Kuhusu
uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa mkoa kwa ujumla ,Wasira amesema yapo
mengi yanayotarajiwa kufanyika ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bandari ya
Musoma sambamba na kuimarishwa kwa sekta ya kilimo kwa kujenga
miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili wananchi waachane na kilimo
cha kutegemea mvua.
"Kwakweli
mambo ni mengi nikianza kutaja kila kitu hapa basi tutalala Mukendo
itoshe kusema tuna mipango mizuri sana na nyie, tutakwenda kufufua
viwanda na kila kitu ili mradi uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa mkoa
uimarike," amesema
Wasira
amesema licha ya uwepo wa watu wanaodai kuwa chama hicho hakijafanya
chochote katika maisha ya watanzania lakini ni ukweli usiopingika kuwa
maendeleo mengi yamefanyika na ndio maana chama hicho kinaendelea kupata
ujasiri wa kuomba ridhaa kwa wananchi.
"Tukisema
tuwafufue wale waliokuwepo hapa miaka ya 61 hakika wakija watasema hii
sio Musoma kwani maendeleo ni mengi sana mfano miaka minne ya Samia
amejenga shule mpya za Sekondari tatu, madarasa 98 ya shule za Sekondari
na madarasa 68 katika shule za Msingi, kituo kimoja cha afya na
zahanati tatu," amesema
Akifungua
mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini, Benedict Magiri
amesema wana CCM ndani ya wilaya hiyo wana mshikamno kwa asilimia 89
baada ya kuvunjwa kwa makundi yaliyotokana na mchakato wa kura za maoni
ndani ya chama hicho.
"Tumepita
kwenye kata zote 16 za Manispaa ili tusemane,tuzungumze na tuwekane
sawa lengo kuu likiwa ni kuvunja makundi ili wana CCM tuimbe wimbo mmoja
wa Chama cha Mapinduzi,' amesema
Amesema
anaamini kwa vikao hivyo walivyofanya wanachama wa chama hicho sasa
hivi wameshikamana na kwa pamoja wanatafuta kura za chama kuanzia urais
hadi udiwani.
Mgombea
ubunge wa Musoma Mjini, Mgore Miraji amewaomba wakazi wa jimbo hilo
kukipigia kura chama cha Mapinduzi huku akisema changamoto zote za
wakazi wa jimbo hilo zinakwenda kupatiwa ufumbuzi.
"Changamoto
kubwa ya Musoma ni ajira na uchumi niwaombe nyie mniachie hilo jukumu
nyie kazi yenu ni kumchagua Mgore, mama Samia na madiwani wote wa CCM
halafu muone tutakayofanya," amesema
Mgore
amesema ili kupata suluhisho la kudumu katika changamoto hizo suala la
uwekezaji na ufufuaji wa viwanda litapewa kipaumbele huku akisema kazi
ya kuwatafuta wawekezaji ataifanya yeye mwenyewe na kuiomba serikali
kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Mara, Iddi Mkowa amesema chama hicho kinaamini katika
utawala wenye kuzingatia usawa wa wa kijinsia kwa vitendo na kwamba
katika kuhakikisha hilo linafanikwa wagombea ubunge katika majimbo manne
kati ya kumi yaliyopo mkoani humo ni wanawake.
Ameyataja
majimbo hayo na wagombea wake kuwa ni pamoja na Mgore Miraji(Musoma
Mjini), Mary Daniel (Serengeti), Esther Matiko (Tarime Mjini) na Esther
Bulaya (Bunda Mjini).
Mwenyekiti
mstaafu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT), Gaudensia Kabaka
amesema hii ni mara ya kwanza kwa chama hicho kusimamisha wagombea wengi
wanawake kwa nafasi ya jimbo mkoani Mara.
"Hii
haikuja kwa bahati mbaya wote tunajua Mkoa wa Mara ulikuwa na sifa gani
kuhusu wanawake lakini kazi imefanyika na kwasasa tunaona matunda,
niipongeze kamati kuu kwa kazi nzuri haikuwa rahisi lakini hakika
wameweza," amesema
Amesema
wagombea wote walioteuliwa na chama hicho wana sifa na wanafaa kuwa
wawakilishi wa wananchi huku akiwataka wakazi wa Mkoa wa Mara kujitokeza
kwa wingi kukichagua Chama cha Mapinduzi Oktoba 29,2025.
Mgombea
ubunge Tarime Mjini, Esther Matiko amesema Mkoa wa Mara umeongoza
nchini kwa kuteuwa idadi kubwa ya wagombea wanawake kwenye majimbo jambo
ambalo halikuwahi kutokea huko nyuma.
Amesema
uteuzi wa wagombea wanne wa nafasi hiyo katika majimbo hayo ni sawa na
asilimia 40 na kwamba katika historia ya mkoa huo haijawahi kutokea
kuwepo kwa wagombea wengi wanawake na kuahidi kuwa endapo watachaguliwa
watashirikiana na wabunge wengine pamoja na madiwani wote kuhakikisha
ilani ya CCM inatekelezwa kwa asilimia 100.
"Mara
huko nyuma tulikuwa tukitambulika kama mkoa ambao hauthamini wanawake
hasa kwenye masuala ya uongozi lakini CCM chini ya Rais Samia
imeidhihirishia dunia kuwa Mara tunaweza kilichobaki ni kupiga kura ili
tufanye kwa vitendo," amesema Matiko
Aliyekuwa
Mbunge wa Musoma Mjini, Vedastus Mathayo amesema hana shida na maamuzi
yaliyofanywa na chama chake kwa maelezo kuwa chama hicho ni kikubwa
zaidi ya mtu binafsi.
Jina
la Mathayo lilikatwa katika hatua za awali kabla ya mchakato wa kura za
maoni jambo ambalo kwa namma moja ama nyingine lilisababisha makundi
ndani ya chama hicho katika jimbo la Musoma mjini.
"Wanaosema
nina kundi sio kweli kwanza mimi sikuwa mgombea lakini pia najivunia
kufanya kazi na marais wanne na muda wote tumeleta maendeleo
yanayoonekana kwa macho na ni kwa faida ya jimbo letu hivyo sina
kinyongo na maamuzi ya chama changu zaidi najivunua maendeleo
yaliyopatikana wakati wa uongozi wangu," amesema
Mathayo
amesema chama chao ni kama kocha wa mpira wa miguu ambaye anaamua
ampange mchezaji gani kwa wakati gani hivyo mchezaji hawezi kuhoji
kwanini hajapangwa kucheza.
"Mchezaji
usipopangwa kuna mawili aidha kiwango chako kimeshuka au umewekwa akiba
ila mimi naamini nimewekwa akiba kwahiyo sina wasiwasi wala kinyongo,"
amesema
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira,
akimuombea kura Mgombea wa Ubunge jimbo la Musoma Mjini Ndg. Mgore Miraji Kigera katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mkendo Musoma.
fanya ku Subscribe BukobaWadau Live kwa matukio ya Papo hapo Gonga HapaCHANNEL BUKOBAWADAU LIVE
BukobaWadauLive – Ushuhudie Kagera kwa mtindo wa kisasa!
1. 🎉 Sherehe, Ngoma Zetu na Burudani
2. 💍 Harusi za kitamaduni na sherehe za familia
3. 🕊 Kumbukizi & Matanga
4. 🏞 Vivutio vya utalii & historia
5. 📖 Simulizi za kiutamaduni
6. Mtaa kwa Mtaa
💡 Jiunge sasa, subscribe 🔔 – usikose tukio lolote LIVE