Bukobawadau

HISTORIA NYINGINE JIMBO KATOLIKI LA BUKOBA ASKOFU DESIDERIUS RWOMA ASIMIKWA RASMIi

Jimbo Katoliki la Bukoba (kwa Kilatini Dioecesis Bukobaƫnsis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa linahusiana na Jimbo kuu la Mwanza
Bukobawadau tumeshuhudia  Askofu mpya akisimikwa  Rasmi na kuwa katika ushirikiano mkubwa na msaidizi wake Askofu Method Kilaini.

Ibada ya kumsimika rasmi Askofu mpya ikiendelea,Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desiderius Rwoma, kabla ya uteuzi/uhamisho, Rwoma alikuwa askofu wa Jimbo la Singida. Wasifu Askofu Desiderius Rwoma alizaliwa mwaka 1947 katika Parokia ya Rutabo, Kamachumu jimbo Katoliki la Bukoba. Parokia moja na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa. Alipata upadrisho kwa mikono ya Askofu Timaywa, mwaka 1974 pale Rutabo. · Akiwa jimboni Bukoba aliwahi kuwa gambera (Mkuu wa shule) ya seminari ya Rubya kwa miaka mingi. Wakati wake shule ya Rubya mara kadhaa ilikuwa ya kwanza kitaifa katika mitihani na karibu mara zote ilikuwa kila mara kati ya shule 10 bora taifani
Mapadre wengi vijana jimboni Bukoba walipitia mikono yake hivyo anawajua vizuri na wanampenda. · Vile vile alikuwa mlezi wa kiroho wa shirika la masista wa Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu, shirika la jimbo na hivyo analifahamu vizuri na kila mara amekuwa karibu nao. · Kabla ya kuteuliwa kuwa askofu wa Singida alikuwa makamu wa askofu na hivyo kulijua jimbbo la Bukoba na uongozi wake. Alifanya kazi hii vizuri sana na hivyo kuteuliwa kuwa askofu wa Singida. · Akiwa askofu wa Singida (1999 – 2013) ameonyesha karama zake za uongozi. Ameweza kuleta maendeleo ya kichungaji na kibinadamu katika jimbo. Ameonnyesha uelewano wake kwa kuwaalika mashirika mengi ya kitawa ambayo kila moja limeleta karama yake ya maendeleo, uchungaji, shule, vituo vya afya, maendeleo ya akina mama na vijana nk. · Katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anasimamia idara kubwa ya Utume wa walei Askofu Desiderius Rwoma akaelezwa na Askofu Msaidizi, Methodius Kilaini kupitia Mtandao wa Bukoba Group, kuwa ni mpole, mnyenyekevu, msikivu, muwazi na mpenda maendeleo. Ana uhusiano mzuri na kila mtu bila kujali hali, jinsia, kabila, taifa au dini.
 Shughuli hii ya kumsimika  Rasmi Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba imehudhuliwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh Benjamini Mkapa (pichani katikati) ,Katika salaam zake Mh . Mkapa amesema;' Wakati wa uongozi wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuhudumia makundi yote bila ubaguzi,Ata wananchi sikuwasikia wakitowa malalamika ya kubaguana!!'
MKAPA miongoni mwa mambo ninayojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote.
 Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa katika Shughuli ya Ibada ya Kumsimika Rasmi ASKOFU DESIDERIUS RWOMA iliyofanyika Katika Kanisa kuu Jimbo Katoliki la Bukoba.
Waumini wakiendelea na Ibada
 Baadhi ya waumini wa wakikatoliki  wakielekea katika kutoa sadaka wakati wa ibada ya kumsimika Rasmi Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Askofu Desiderius Rwoma.



Waumini wakitowa zawadi kwa Askofu mpya, Askofu Desiderius  Rwoma

Nje ya viwanja vya Rumuli ambapo imefanyika hafla ya kumkaribisha Askofu mpya, Pichani anaonekana Askofu Kilaini Akibadilishana mawazo na Mdau.

Askofu Nestory Timanywa anayestaafu uaskofu wa jimbo hilo baada ya kutimiza umri wa miaka 75 kwa mujibu wa sheria za kanisa.
 Historia mpaka leo kwa Maaskofu wa Bukoba
Mpaka hii leo historia ya Maaskofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba inasomeka hivi;
  •  Askofu Mpya  Askofu Desiderius Rwoma  (mwaka 2013)
  •  Askofu Nestorius Timanywa (tangu tarehe 26 Novemba 1973)
  •  Askofu Placidus Gervasius Nkalanga, sasa O.S.B. (6 Machi 1969 – 26 Novemba 1973)
  •  Kardinali Laurean Rugambwa (21 Juni 1960 – 19 Desemba 1968)

 BUKOBAWADAU BLOG, WANABUKOBA NA WANAKAGERA KWA PAMOJA TUNAKUKARIBISHA ASKOFU RWOMA KWA UPENDO FURAHA NA SHANGWE, TUNASEMA KARIBU NYUMBANI!!!
PATA HABARI ZA PAPO HAPO KUPITIA FACEBOOK PAGE YETU, PIA WAWEZA KUWASILIANA NASI KUPITIA VIBER 0784 505045,BBM PIN  234E5DD7,SIMU NO.0715 505043/0754 505043 Email bukobawadau@gmail.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau