Majaji mbalimbali pamoja na majaji wastaafu wakiongozwa na Mwakilishi wa Jaji Mkuu kuwaongoza maelfu ya wananchi ,Viongozi mbalimbali wa Serikali ,taasisi pamoja na familia ya Prof John Ruhangisa katika shughuli ya Mazishi ya Marehemu Letitia R. Ruhangisa.
Marehemu Letitia R. Ruhangisa alifariki dunia Oct 29,mwaka huu katika ile ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Makumira wilayani Arumeru baada ya basi dogo aina ya Hiace kugongana uso kwa uso na lori la mafuta na kuwa miongoni mwa watu 12 waliopoteza maisha siku hiyo.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Letitia K.Ruhangisa mara baada ya kutolewa nje tayari kwa Ibada iliyofanyika Nyumbani Kijijin Ibwera -Kibona Bukoba Vijijini
Mme wa Marehemu Letitia K. Ruhangisa ,Prof John Ruhangisa na wanae watatu Mollen, Fiona na David pichani kulia wakati wa Ibada.
Ibada hiyo ikiongozwa na Padre aliyesomeshwa na familia hii akishirikiana na Mapadre wengine ya kadhaa
Mollen Ruhangisa akisoma neno.
Taswira mbalimbali wakati Ibada ya Mazishi ya Letitia K. Ruhangisa ikiendelea
Katikati anaonekana Jaji Rutta
Waumini wakiendelea na Ibada.
Hakika ni masikitiko makubwa kwa Prof John Ruhangisa na familia yake
Mzee James Lugemalira na Mr Eniki Kashasha wakati wa Ibada
Mr. Basibila wakati Ibada ya mazishi ikiendelea.
Polisi wa Usalama barabarani kama walivyokuwa sehemu ya maegesho
NduguNovatus Nkwama mwenyekiti wa wilaya Bukoba vijijini ccm
Taswira eneo la tukio
Dada Messe na Bi Jeanifer Murungi Kichwabuta
Ibada imegudhuriwa na watu wengi sana kutoka maeneo mbalimbali
Sehemu ya wanafamilia anaonekana 'Mnyaluganda' Bi Maua Ramadhani.
Sehemu ya Ndugu wa familia.
Kulia anaonekana Sakina Sinda, Wakili wa Serikali Mfawidhi - Mkoa wa Kagera
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera
Prof Boniventure Rutinwa akiendelea kuratibu shughuli hii kutokana na ratiba ilivyo.
Kijana David ambaye ni Mtoto wa Marehemu Letitia, utapata kuona na kusikia alichokisema kupitia video yetu iliyopo mwishoni mwa ukurasa huu.
Salaam za ambirambi kutoka kwa Wanajumuhiya
Taswira mbalimbali shughughuli ya Ibada ikiendelea.
Mh. Jaji Lutta akitoa salaam za rambirambi kama mwakilishi wa Jaji Mkuu aliyehudhuria katika Ibada ya kuaga huku Arumeru kabla ya Safari kuelekea Bukoba
Camera yetu katika kuangaza huku na kule wakati shughuli ikiendelea..
Muda mchache kuelekea eneo la makabui.
Jeneza likiwa kaburini.
kutoka kusgoto anaonekana Mr Siza , Mr Aniki Kashasha na Mzee Adv. Ishengoma wakishiriki shughuli ya mazishi haya.
Msalaba ukisimikwa Kaburini
Askofu Mkuu Mstaafu na kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,Dk.Samson Mshemba
Askofu Mkuu Mstaafu na kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (
Prof John Ruhangisa pichani akiwa tayari kuweka shada la Maua katika kaburi la Mke wake mpendwa Letitia K.Ruhangisa
Watoto wa Marehemu na Baba yao kwa pamoja wakiweka
Shada la maua kwa niaba ya wanaukoo wote.
Kwa niaba ya wanaukoo na kama rafiki wa familia, anaonekana Mzee James Lugemalira katika utayari wa kuweka shada la maua.
Mzee James Rugemalira akiweka shada la maua
Bi Jeanifer Murungi Kichwabuta akiweka shada la maua
Matukio ya mbalimbali heshima ya Mwisho ya Letitia K.Ruhangisa
Mama Adventina Matungwa akuweka shada la maua
Mdau Mama Stella.
Mr. Kashasha katika hili na lile na Ndugu Rahym Kabyemela.
Mama Matungwa pichani kushoto
Mdau Deo akiteta jambo na Ndugu Cathbert Basibila.
MATUKIO ZAIDI YA PICHA YANAENDELEA HIVI PUNDE NA SEHEMU YA VIDEO..
Mama Abayo pichani
Mr Prudence karugendo akiwajibika katika Msiba huu mkubwa wa Dada yake Mpendwa
PITIA SEHEMU YA VIDEO HAPA CHINI IBADA YA MAZISHI YA LETITIA RUHANGISA KWA PICHA ZAIDI INGIA HAPA >Bukobawadau Entertainment Media
BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
4 comment:
Tunakushukuru sana Ndugu Baraka kwa kutuwezesha kufuatilia mazishi ya mpendwa mdogo wetu Koku. Hatukuwepo kimwili lakini tulikuwepo pamoja na wafiwa.
Mungu ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema peponi, Amina.
Ajali za barabarani zinalitekeketeza taifa kila kukicha na trafiki tunawaona wengi tu barabarani.
Nadhani wanaotumaliza ni trafiki na sio ajali. Makosa ya barabarani ni neema kwa matrafiki sababu wanapoona kosa wanajua watapata pesa na sio kusahihisha kosa! Tunachotakiwa kufanya wananchi ni kuwadhibiti matrafiki ili nao wakayadhibiti makosa yanayofanywa na waendesha vyombo vya moto barabarani. Kimojawapo ambacho tungekitumia kama kigezo ni vitambi. Kila trafiki mwenye kitambi ajieleze amekipataje wakati anashinda juani kuangalia usalama barabarani. Vipato vyao vinaeleweka, kwahiyo tuangalie mali walizonazo kwa kuzilinganisha na vipato vyao halali. Vikitofautiana tuelewe utajiri walio nao unatokana na kuziweka roho zetu rehani. Tusipochukua uamuzi huo tujue imekula kwetu, matrafiki wataendelea kunenepeana na kujirundikia utajiri huku wananchi tukizidi kupukutika kwa ajali za barabarani.
Nadhani ni jambo la kukubali kazi ya Mungu...mara nyingi tunasema ebya akagonza bibe omunsi nomuigulu...chonkai akanya konai konai kabitwijaho twishanai abalikulogotai...kwa hakika ina uma sana..sim fahamu huyu dada lakini kwa ujumla wake wote tumesikitika sana, na hasa wale wa karibu yake!!
mambo ya barabara na trafiki hakina tusiende huko....sasa ndege ikianguka...tutasemaje!!
Hapa Tanzania, ajali za barabarani zinazosababishwa na tabia mbaya (bad driving behavior) na makosa ya kibinaadamu tu, zinaendelea kutumaliza. Tumepoteza wapendwa wetu wengi, tumepoteza hata viongozi wakuuu serikalini wakiwemo mawaziri, sisi wengine tuna vilema vya kudumu kwa sababu ya ajali. Lakini bado hakuna hatua sahihi zilizochukuliwa ili kukabiliana na matatizo ya ajali za barabarani. Hivi karibuni, vyuo vikuu vimekuwa na tafiti kadhaa zinazogusa usalama barabarani. Maandiko na machapisho kadhaa yamefanyika. Mikutano mikubwa (Conferences) zimefanyika, ukiwemo ule mkutano wa wahandisi uliofanyika Arusha 2011 ambapo mimi binafsi niliandika na paper iliyosema – “ICT as a tool for development of traffic control systems”. Pale tulitoka na maazimio yaliyopelekwaa serikalini, lakini ukipima utekelezaji wake au dalili tu za utekelezaji, huzioni. Kwa hili la ajali, ni tatizo!!
Ukirejea kwenye historia ya nchi nyingi, jinsi gani walivyoweza kukabiliana na matatizo yanayosababishwa na ajali za barabarani, utaona kuwa sio serikali iliyo kuja na ufumbuzi wa matatizo, bali ni vikundi vya kijamii. Jamii zinazohusisha watu wote, wa fani zote, kwani sio trafiki wa usalama barabarani wanaopata madhara, ni wasafiri wenyewe. Trafiki huja tu kupima, kuchukua maelezo na kuendesha kesi upande wa dola. Kesi haikuondolei maumivu ya kuumia physically, haikuondeli maumivi ya kuwapoteza wapendwa wetu na haikuondolei ukiwa.
Hivyo basi ni wananchi wenyewe walioleta jawabu kwenye nchi za wenzetu kupitia “Pressure Groups” zao.
Hivi kweli kwa wale wanaotumia viapo, ni nani anaweza kuapa ambele ya mwenezi Mungu, muumba wa wote, kuwa “Nakiri kwa moyo na natamka kwa ulimi kuwa askari wa usalama barabarani wanatekeleza majukumu yao vizuri, hawadai na kuchukua pesa kutoka kwa madereva”?
Nimepitia machapisho mbalimbali na kubaini kuwa, ni wasafiri wenyewe wanaweza kushinikiza serikali kuleta mabadiliko ya kweli dhidi ya mwenendo na tabia mbaya ya uendeshaji magari hapa Tanzania. Kweli inauma sana kuona kuwa hali kama hii inaachwa tu iendelee. Mimi kama raia ninayepitia sana machapisho ya vipimo, ni kipimo kimoja tu sijawahi kukiona. Nacho ni kile kipimo kinacho fananisha/pima kwa kulinganisha kitu chochote kile dhidi ya maisha ya binaadamu .
Post a Comment