Bukobawadau

Miembeni Yatinga Nusu fainali:Yashinda 1-0 dhidi ya Hamugembe

Mchezaji wa kutumainiwa Ramadhani Yusuph(kapilima)
Pichani ni Athmani ally(Chuji),Omary na Hassan

Wakati wakijipanga kwa ajili ya mpambano,hapo wapo Smart hotel walipoweka kambi ya siku moja.
Mwenye mpira Ni Brother men Dulla

Kiongozi wa timu ya Miembeni Abdulrazak Majid katikati na ni mtangazaji wa kipindi cha michezo 88.5 Kasibante Fm Radio

Sehemu kubwa ya uwamasishaji na kiongozi mwenye Suti Ni Jamal Kalumuna (Jamco)Mkurugenzi wa Jamco video Production.
Mpira ni pamoja na vifaa kama unavyo jionea ndg mdau(kwa mtaji huu kwa nini ushindi usipatikane?!!!!)
Katikati ni Bi Zakia Kassim mdau wa soka na mwanaharakati wa Miembeni Fc,picha ya pamoja na viungo machachari!!!!

Mwanadada Mainda Kassim kama kiongozi wa timu akiwa pamoja na Mchezaji tegemezi Ramadhan Yusuph (Kapilima)

Mh Diwani kata ya Miembeni Ndg Richard akiwa na mchezaji wa timu yake mda huo bado wapo smart hotel!!!

Kabla ya kutoka hotelini Walitanguliza dua kama unavyojionea!!

Katikati ni kipa mahili wa Miembeni Ndg Maulid

Wa mwisho kulia ndiye Mwalimu anaye kisuka kikosi cha Miembeni mpaka kikawa gumzo Ndg Cletus Mtakyawa
Dakika chache kabla ya kuingia uwanjani Kaitaba wachezaji na viongozi wao walipita mitaa ya ziwani kidogo kama utaratibu waliojiwekea

Mwisho wa siku Miembeni wakaibuka kidedea kwa ushindi wa Bao 1-0 na hapo wanaonekana wachezaji wakipongezana.

Ushindi huu unawakutanisha Miembeni na Kashai katika nusu fainali,pichani ni Ndg WillY kiongozi wa kashai akionyesha kuwapa saport mahasimu wake ile hali akijua kuwa kazi iliopo mbele yake si ya kitoto!!!

Bukobawadau tunatoa shukrani kwa Mainda Kassim kwa kuweza kwake kutufikishia picha hizi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau