Bukobawadau

WAASI WAIDHIBITI TRIPOLI


Tripoli imeshuhudia mwendelezo wa mapigano na vikosi vinavyomtii Gaddafi katika mji wa Tripoli siku moja baada ya waasi kuteka makazi ya Gaddafi.

Kumekuwa pia na makombora mapya ya NATO.

Waasi walipigana na wanaomuunga mkono Gaddafi katika maeneo kadhaa ya kusini na katikati ya mji, kikiwemo kikosi kingine kutoka mashariki mwa uwanja wa ndege.

Mlipuko wa mabomu mawili ulitikisa mji wakati ndege za NATO zilipopita angani.

Haijulikani Kanali Muammar Gaddafi aliko lakini alitoa ujumbe wa kutokujisalimisha jana usiku.

Katika ujumbe wake, amesema alifanya ‘mbinu’ kurudi nyuma kuondoka kwenye makazi yake ya Bab al-Aziziyalakini mwanadishi wa BBC BBC Wyre Davies anaripoti kutoka mjini humo kuwa hakuna anayeamini ripoi ya matukio hayo.

Wadunguaji wanaomuunga mkono Gaddafi walionekana ndani ya Bab al-Aziziya yenyewe baada ya kuvamiwa na waadi na vita ya kuidhibiti kikamilifu Tripoli inaendelea.

Kanali Gaddafi inadhaniwa kuwa ana wafuasi wengi katika miji mikubwa miwili ya Sirte ulio pwani na Sebha kilometa 650 (400 maili ) kusini mwa mji, ambako mapigano yalizuka wiki hii.

Wakati huo huo, Baraza la waasi la Mpito (NTC) likimaanisha kuanza kazi ya kuijenga upya Libya iliyosambaratishwa na vita, linafanya kikao na wafadhili nchini Qatar huku ujumbe wa maafisa ukihama kutoka ngome ya waasi ya Benghazi kwenda Tripoli
.
Waasi wakishangilia mjini Tripoli
Next Post Previous Post
Bukobawadau