Bukobawadau

JOSIAH GIRLS' HIGH SCHOOL:Ni Shule mpya ya Wasichana inayo Ongoza kwa kutoa Elimu Bora Mkoani Kagera

Siku ya Ziara ya Baba Askofu Mh Dr.Malasusa Askofu Mkuu wa KKKT,Shuleni Josian Girls High School.
Ziara ililenga kuongea na walimu pamoja na wanafunzi
Hii ni Picha ya pamoja Askofu, Wafanyakazi,Wanafunzi na Wakurugenzi
.
Wanafunzi wa Pre form one wakimwonyesha Askofu Mkuu Dr Malasusa uwezo wao kutumia kompyuta.
Baba Askofu akipanda Mti wa kumbukumbu shuleni Josiah Girls' High School.
J0SIAH GIRLS' HIGH SCHOOL
Hii ni Shule ipatikanayo ndani ya Manispaa ya Bukoba.
Iko nje kidogo ya mji umbali wa kilometa 6 jambo ambalo linawezesha wanafunzi kusoma kwa utulivu.
Vilevile ipo katika ukanda wa milima mizuri inayo pokea upepo mwanana kutoka ziwa Victoria.
Shule hii imepakana na chanzo cha chemichemi ya Kitela yenye maji safi yasio kauka

Wanafunzi wa JOSIAH picha ya Pamoja na wajerumani katika Ziara yao ya kufanya Tathmini.
Haya ni Mazingira ya shule
Shule hii inatoa masomo ya kompyuta
Ziara ya wazungu kutoka Ujerumani.
Walimu wakipanda Mti
Pia Wageni kutoka Ujerumani walivutiwa na uwezo wa wanafunzi wa Pre form one wa kutumia Kompyuta.

KAULI MBIU YA SHULE HII NI:Ndoto yangu,upeo wangu.

-Shule imesajiriwa na Wizara ya Elimu na M afunzo ya U fundi.
Namba ya usajiri ni S.4273 na namba ya kituo cha mtihani ni S.3241

-shule hii inatoa huduma ya kuandaa wanafunzi wanaohitaji kujiunga na kidato cha kwanza kwa masomo ya Kingereza,Hisabati na Kompyuta.

-Inatoa Elimu kwa wanafunzi wa kidato cha I-IV kwa masomo ya Sanaa,Sayansi na Biashara.

-Shule hii inatoa mafunzo ya kidato cha V-VI katika michepuo ya HGK,HGL,HGE,EGM na HGL.

-Shule inao walimu wenye sifa,madarasa,maktaba,kompyuta,mahabara,viwanja vya michezo,mabweni pamoja na usalama wa kutosha.

ANWANI YA SHULE

Mkuu wa Shule,
Josiah Girls' High School
P.O.BOX 1605
BUKOBA-TANZANIA

Barua pepe:josiahgirls@yahoo.com

simu:+255 782 300 258
+255 762 261 885
+255 768 572 163

Fax: 028 22210101
Next Post Previous Post
Bukobawadau