Bukobawadau

AJALI YA YATOKEA USIKU HUU ;Gari la gonga hodi Nyumba ya Masjid KSI Jamaat-

Gari aina ya Forester ikiwa imeama barabara na kugonga mlango wa Nyumba kana kwamba ndio imefika inapo takiwa kufika,tukio hili limetokea ar majira ya saa 5 usiku.
Nambari za gari ni T389 BNG mali ya bwana Kipara mfanyabiashara.
Papo kwa papo Camera yetu ilifika kwenye tukio na kukuta mzozo mkubwa kati ya wadau na askari wa barabarani kwa kile kilichosemekana kuwa mhusika kaachiwa kitu ambacho bukobawadau atukuweza kudhibitisha kutokana na upande wa pili kudai mhusika tayari yupo kituo cha polisi,
Kuingia ndani ya Nyumba nimekutana na hali hii na zikisikika sauti za watoto wadogo wakilia kwa mahadhi ya kidosi
Sikuweza kujua mojamoja kilicho kua kikiendelea ndani ila mdau unaweza kupima uzito wa tukio na hali ya mazingira
Mzee Ali pichani Baba wa familia katika nyumba hii akinionyesha hali ya vitu vilivyo alibika.
Nyumba hii ipo kati ya makutano ya barabara ya Kashozi na barabara ya Arusha,maarufu kama maeneo ya kengere tatu.

Nyumba hii inamilikiwa na Msikiti wa KSI JAMAAT.
Hii ni bukobawadau blogspot kwa matukio ya hapa na pale mjini hapa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau