Bukobawadau

KAMACHUMU YETU HII LEO;Mji wenye historia Ndefu Chimbuko la Cardinaly Rugambwa,Askofu Kibila,Hapo Hapo ndiyo Tanulu la siasa,Wadau Wengi hapa ni Watata ile mbayaaaa!!!


Katika pita pita zangu hii leo nikiwa anga za kamachumu km 2 kabla ya kuingia mjini Milama,Nalazimika kufika kwenye nyumba ya mushonge nipati walau picha na uhalisia wa ndani.

Nyumba ipo katikati ya shamba zuri la migomba yenye afya!!!
Ikiwa kwenye mazingira safi imewekewa uzio wa matete(embingo kama wasemavyo wao)nakumbuka enzi hizo matete yakitengeneza vitanda vya kulalia binafsi nimepitia maisha hayo.

Baadhi ya viunga vya Kamachumu hii leo.


Yaap moja kwa moja nakanyaga kwenye mji wa Kamachumu,Mji wenye hekaheka nyingi,wadau wengi ni watata sana,Mji huu ndiyo chimbuko la maaskofu wakubwa na maarufu tukianza na Askofi Kibila na hapo hapo anazaliwa Cardinal wa kwanza wa Afrika Cardinal Laurean Rugambwa,pia Askofu msaidizi Titus Joseph Mdoe wa Jimbo kuu la Dar es Salaam ...kijiji cha Muutwe na Baba ni Mzaliwa wa kijiji cha Katoma- Kamachumu 
Watu maarufu walitokea hapo akina,
Prof Lwakabamba,  Anthony Rugangila,Kalinjuma,na Ntonini,Haji Hamad,Byabusha,Mzee Songoro aka Karasha,familia ya Bukenya alikadhalika Zakalia Mugyabuso Petro Nshange aka (kibunda) na Christopha Ngaiza wote ni marehemu
Majemedali wengi kama bora Imani,Haji Birundulu na Haji Kabalala,Mzee Kabea na Haji Hamad nitakua sijatenda haki nisipo mkumbuka Bandeko na familia nzima ya akina Fresh.

Pia ipofamilia ya al-squar ndio akina mawingu ,Adara na wadau wengine wengi hii ni kwa mkutasari tu!!!

Kwa sasa wapo akina Hamed Kiwanuka , Veda Rugabela,Mdau Myaga , Mzee Thadeo Iluganyuma na Mdau Sued ukanda wa Rutabo akiwepo Mzee Nestory Kato, mdau Chamisili na mwalimu Mastura
Hii ni kwa uzoefu wangu wa mazingira mie Mc baraka blogger bukobawadau.
Next Post Previous Post
Bukobawadau