Bukobawadau

KINGWNGALLAH HAMIS(MBUNGE )SIKU ZAKE ZINAHESABIKA NDANI YA CCM

Jana jioni majira ya saa 10, kikao cha kamati ya wabunge wa chama cha mapinduzi ilikutana Dodoma kujadili mambo mbalimbali na hapo ndipo suala la mjadala wa sakata la madaktari ililipoibuliwa na Mbunge wa Nzega kuhusishwa na mgomo huo.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinasema wabunge wa CCM ambao ni mawaziri walipata nafasi ya kumsulubu Kingwangallah kama wanavyotaka ukizingatia kuwa amekuwa akiwabana sana mara kwa mara akiwa bungeni kutokana na misimamo yake ya kutetea haki na ukweli. Mhe. Adam Kighoma Malima alikuwa wa mwanzo kuongea na aliutumia muda wake wote kumshambulia Kigwangallah akidai ndiye aliyefadhili mgomo wa madaktari na ndiye aliyeendesha harakati za mgomo huo mwanzo hadi mwisho.

Pia aligusia kuwa Kingwangallah hakuongoza kura za maoni, alikuwa nafasi ya tatu nyuma ya Bashe na Selelii, lakini chama kilimpendelea na kumpa nafasi yeye. Malima alimtaka Mwenyekiti wa kikao hicho, ambaye ni Waziri Mkuu, amtake Kingwangallah kupanda mbele ya podium na aeleze uhalali wake wa kuwa kwenye kikao cha mgomo wa madaktari na kushawishi wagome na aseme kama yuko CCM ama la! Na kama yuko CCM kwa nini hakuisaidia serikali? 

Baada yake alikuja Mhe. Hawa Ghasia ambaye alimtukana Kingwangallah kuwa ni mbishi, jeuri na hakufunzwa na wazazi wake na kwamba CCM hawatomuweza. Alisema Kingwangallah afukuzwe chamani na yeye (Ghasia) yuko tayari kwenda kupiga kampeni Nzega kuhakikisha jimbo linarudi CCM.

Wabunge wengine waliunga mkono hoja hiyo huku wakionesha kusikitishwa na hatua ya Mbunge huyu kushiriki kwenye mgomo wa madaktari na kuwahamasisha kuibana serikali mpaka kieleweke! Mbunge Kingwamngallah alionekana kukosa support ya wabunge kabisa na hata wale walioonekana kumuonea huruma walinyamaza na hawakutaka kuonekana wazi wazi kabisa kuwa wako na Kingwangallah.

Mawaziri walimshambulia mpaka basi tu. Kikao kiliazimia kupeleka mapendekezo ya kumfukuza kwenye kamati ya uongozi. Kikao hicho kimekaa leo jioni kuanzia saa 10. Bado hatujajua wameazimia nini mpaka sasa. Je akifukuzwa ataenda Chama gani? Bado hiyo haijajulikana...ila taarifa kutoka kwa watu walio karibu naye zinasema kwamba ameamua kujiuzulu kabla ya kusubiri kufukuzwa. 'Tayari ameishaanda barua na anasubiri tu kuitwa ili aiwasilishe.
Chanzo Jamii Forums.
Next Post Previous Post
Bukobawadau