Bukobawadau

KANISA LA ANGLIKAN BUKOBA LATOA MSAADA WA FEDHA KWA WATOTO YATIMA NI FRORIDA AUDAX(19) NA MDOGO WAKE VENANCE KALOKOLA AUDAX NA BADO MSAADA UNAHITAJIKA


Muwakilishi wa kanisa la Anglikan Ndug Emmanuel Bililiza akimkabizi mtoto Frolida Audax (19) fedha tasilimu ndani ya ofisi za kasibante FM katikati ni mdogo wake Venance Audax
 FRORIDA AUDAX(19) akiwa na mdogo wake VENANCE KALOKOLA AUDAX.
Manager wa Radio  kasibante FM ndugu Emmanuel Mbaule akiwa ofisini kwake na ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kueneza habari  za watoto hawa
 Picha ya Pamoja wafanyakazi wa kasibante FM pamoja na mwakilishi wa kanisa la Anglikan
Bi Abella Kamala(kulia)afisa masoko kasibante Fm Radio  anazidi kusisitiza kuwa msaada zaidi unatakiwa kwa watoto hawa yatima.
 
Kanisa la Anglikan bukoba leo 19/2/2012 limetoa kiasi   cha shilingi 94,500  ikiwa ni msaada walioutoa kwa watoto yatima florida audax [19] pamoja na venance kalokola audax (7) wa kijiji cha kibuye kitendaguro  mara baada ya kusikia historia ya maisha yao katika kipindi cha dira ya maisha kinachorushwa na kasibante fm radio kila siku ya jumamosi.
 Ikumbukwe kuwa kasibante fm radio iliwahi kurusha matatizo ya hao watoto October 1, 2011, mara baada ya kufiwa na baba yao huku mama yao akiwa anaumwa na hana uwezo wa kuwasaidia. Ni familia ya watoto 4 mkubwa wao wa kike akiwa na miaka 19, anayefuatia wa kike miaka 16,  mdogo wao mwingine wa kike mwenye miaka 10 na wa mwisho wa kiume mwenye miaka 7. Baadhi ya wadau waliwachangia vyakula,mafuta na kiasi cha fedha jumla 120,000/ wadau ambao waliwachangia ni pamoja na LEONARD MTENSA,DIVO RUGARABAMU,VEHICLE INSPECTOR ALEX,MSIKITI WA AHLUL-BAAYT HAMGEMBE, JANE WA MIEMBENI GROCERY, DERICK WA 2 BOYS SHOP MAFUMBO  na wadau wengine.
kwa sasa watoto hawa wamefiwa na mama yao , hawana msaada wa mahitaji na mbaya zaidi nyumba yao ilibomoka wasamaria wakawajengea nyumba kubwa kidogo na katika hali hiyo wakalazimika kumega sehemu ya shamba walioachiwa hivyo wamebaki na shamba dogo sana lenye migomba mitatu tu ambalo halikidhi mahitaji yao ya chakula.
Tunatoa shukrani kwa kanisa la Anglikan Bukoba kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia. Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mchungaji wa kanisa hilo Elisha Bililiza mmoja wa waumini hao Emmanuel bililiza amesema huo ni  mchango wa waumini wa kanisa hilo na wanaangalia uwezekano wa kuendelea kuwasaidia. Msaada huo leo umekabidhiwa mbele ya EMMANUEL MBAULE MANAGER WA RADIO KASIBANTE NA ABELLA KAMALA AFISA MASOKO NA MWENDESHAJI WA KIPINDI HICHO

Radio kasibantena Bukobawadau Blog  tunatoa shukrani kwa kanisa la Anglikan Bukoba na kuwaomba wadau wengine wenye moyo na nia  waendelee kuwasaidia watoto hawa .

Next Post Previous Post
Bukobawadau