Bukobawadau

Mechi ya kirafiki ya Darts kati ya Mwanza na Kagera kwenye Viwanja vya Bukoba Club.

Mgeni Rasmi Mh. Massawe akitoa neno na kukubari kuwa mlezi na mwanachama wa Darts Mkoa wa Kagera
Mzee Rapha kushoto na afisa utamaduni wa Manispaa ya Bukoba Ndg Rugeiyamu kulia.
Mh. Dismas mchezaji wa timu ya Kagera.
Wachezaji wa timu ya Mwanza.
Ndg Sweetbart Mdau wa mchezo wa Darts.
Mechi hii haikuja kama uyoga au senene hapa mkoani Kagera ni juhudi za mpambanaji wa kimataifa Umary MTAJIJU,mdau huyu ndiye juhudi zake zimeleta haya,tumeweza kupata mchezo na jirani zetu Mwanza,tumefahamiana tumeongeza marafiki,tumetengeneza Daraja kati yetu na Mwanza kimichezo hasa Darts Bukoba wadau tunampongeza sana MTAJIJU,amepambana amesajili timu ya darts,kasababisha chama pia kisajiliwe,kaweza kuandaa mchezo wa ujirani mwema,pichani inaonekana timu ya Mwanza pia kuna timu ya kagera ikiwa na tshirt nyeupe sare kwa kagera,zote hizo ni juhudi za Mtajiju akisaidiana na mama komandoo Redemta Mwebesa mama Maziku m Bukoba Veteran halisi
Wachezaji wa timu ya Kagera wakifatilia mchezo.
Mchezaji wa timu ya Mwanza akionyesha umakini.

 BUKOBAWADAU TUNAOMBA WADAU WENGINE TUIGE MOYO HUU SIO MAPOMBE TU ASUBUHI MPAKA USIKU UNAPELEKWA HOME UPO KWENYE P/UP NYUMA KAMA GUNIA LA MKAA HUJITAMBUI UNAJIIMBIA KA WIMBO KA ULEWI 'hakunagaaa hakunagaaa',ETI UMETOKA KUPONDA MAISHA,UKIOMBWA 100 YA KUENDELEZA MICHEZO MKALI KAMA SIMBA MZAZI
Next Post Previous Post
Bukobawadau