Bukobawadau

KAMPUNI INAYOTOA MAFUNZO YA UJASILIAMALI SASA WAPO MJINI BUKOBA NI -GESAP CO.LTD NA DIMOD INTERGRATED SOLUTIONS&AWARENESS YA DSM.

Wadau wa kampuni inayotoa mafunzo ya ujasiliamali Tanzania wakiwa mjini hapa hii leo kwa ajili ya mafunzo yatakayoendeshwa kwa muda wa siku tatu kuanzia kesho tarehe 26-03-2011.
Mafunzo yanahusisha wajasiliamali wote wa jinsia zote na rika zote
Mkurugenzi wa GESAP CO.LTD  ndg Wilbroad G. Mutabuzi.
Mdau huyu ndie muamasishaji mkubwa hadi kampuni hii ya  DIMOD INTEGRATED SOLUTIONS&AWARENESS  ya jijini dar es salaam iweze kufika mjini hapa.

Akiongea na bukobawadau blogspot  Mdau Willy amesema ameonelea ni bora wadau wa nyumbani wapate fulsa hii kujifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumu na kusema bidhaa hizo ni kama  Sabuni za maji,sabuni za miche,sabuni za magadi,shampoo aina zote,mishumaa,mafuta ya kujipaka,lotion,kekiza arusi,dawa za usafu majumbani dawa ya kusafishia vigae,wine aina zote,maji ya betri,mikate,biscut za maziwa na za kawaida,mango pickle,clips aina zote na Uyoga.
 Mdau Ndg Charles.
Mdau Wilbroad Mutabuzi na Mdau Jamal Kalumuna.

Aidha Ndg Wilbroad amesema kutakuwa na masomo ya ufugaji na jinsi ya kutengeneza chakula cha mifugo,masomo ya biashara na afya ya binadamu,kusindika bidhaa zitokanazo na mazao yetu.

Goog packing and labeling na vyeti vitatolewa kwa wahitimu baada ya mafunzo ili kumsaidia mjasiliamali kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi pasipo kusumbuliwa.

Semina itafanyika katika ukumbi wa st. Franses Bukoba Mjini (Miembeni) kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana na 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni  na form zinapatikana kwa Tsh 3000

Ada Tsh30,000(thelathini elfu)nadharia na Vitendo

Kwa maelezo zaidi pia simu;
0784 340 393/0767 840 393      Ndg Nicholus Jovin.
0787 493 777/0767 595 998     Ndg Wilbroad Mutabuzi
0713 712 869/0715 795 533     Ndg Didas.
Email:gesapco@yahoo.com na diamodintsolutions@gmail.com

Next Post Previous Post
Bukobawadau