TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani
ya Simu “MKUUPOLISI”
Ofisi ya
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
24 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi
la Polisi Nchini linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake
linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa
uchochezi na chuki kwa wananchi na viongozi wa serikali kwa njia ya
simu ya mkononi akituma SMS kwa lengo la kuchochea fujo, vurugu na
kutoa matusi kwa viongozi hao.
Mtu
huyo amekuwa akifanikisha kazi hiyo kwa kutumia Chips (sim card) 13 za
simu za mkononi ambazo amekamatwa nazo. Jeshi la Polisi linaendelea
kumhoji mtu huyo na ushahidi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Aidha,
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zingine za
wahahlifu kama hao kujitokeza na kutoa taarifa hizo polisi ili wahalifu
hao waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki, wakiwemo watu
wanaowashawishi wenzao kwa njia ya fedha, kuwashauri ama kuwasaidia kwa
namna yeyote ile katika kufanikisha uhalifu huo na kusababisha uvunjifu
wa amani hapa nchini.
Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria za nchi.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria za nchi.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.