Bukobawadau

UMISSETA MKOA WA KAGERA YAHITIMISHWA KATIKA CHUO CHA UALIMU KATOKE - MULEBA

 Wachezaji wa Mpira wa Wavu Wakichuana Vikali
Timu ya Mpira wa Miguu Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Ikipiga Jaramba Tayari Kupambana na Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Karagwe ilichapwa 2-0 Katika Mchezo huo wa Fainali.
 Mpira wa Kikapu nao Ulikuwa Kivutio Kikubwa katika Mashindano ya UMISSETA mkoani Kagera
Aidha mpira wa Pete kwa Wanafunzi wa Kike nao ulipamba Fainali hizo Muleba Ilifanikiwa Kuichapa Ngara 20-5
 Wataalam Wanaiita Mitupo hapa ilikuwa kurusha Mkuki na Vijana walionyesha Uwezo wao
 
Mashindano ya UMISSETA Mkoa wa Kagera yamehitimishwa rasmi jana tarehe 23/05/2013 baada ya kuwakutanisha wanafunzi wanamichezo kutoka mkoa mzima wa Kagera na kushindanishwa kwa siku nne katika michezo aina mbalimbali na kubaini vipaji katika michezo hiyo.
Bw. Kepha Elias Afisa Michezo Mkoa wa Kagera na Mratibu wa michezo ya UMISSETA mkoa, katika kuhitimisha michezo hiyo alisema kuwa, kwa kushirikiana na wataalam wa michezo wameweza kubainisha wachezaji wenye vipaji watakaounda timu ya mkoa wa Kagera.
Aidha, mashindano ya UMISSETA mkoani Kagera baada ya kuhitimishwa rasmi katika Chuo cha Ualimu Katoke wanafunzi waliochaguliwa katika kila mchezo watabaki chuoni hapo katika kambi ili kuweza kupewa mafunzo na kunolewa zaidi ili waweze kushiriki mashindano ya Kanda.
Mashindano ya Kanda Ziwa Magharibi yatanatarajiwa kuanza Juni 2, 2013 kwa kuhusisha mikoa ya Kagera na Kigoma na yatafanyikia mkoani Kigoma. Baada ya hapo wanafunzi watakaochujwa wataunda timu ya Kanda itakayoshiriki mashindano ya UMISSETA kitaifa mkoani Pwani.
Mashindano ya UMISSETA mkoani Kagera yameongeza chachu ya vipaji vya wanafunzi kwani watoto hao kutoka kila Wilaya waliweza kuonesha vipaji vyao katika michezo mbalimbali. Wilaya ya Biharamulo iliweza kutetea ubingwa wao katika mpira wa Miguu kwa kuichapa Wilaya ya Karagwe bao 2-0.
Wilaya ya Muleba ilweza kuongoza katika mpira wa pete na kufanikiwa kuichapa Wilaya ya Ngara 20-5. Pia Wilaya ya Ngara iliweza kuonyesha ujuzi wake katika mpira wa Kikapu ambapo iliweza kuionyesha ujuzi Wilaya Karagwe katika mchezo wa fainali na kuichapa vikapu 57-37
Kivutio kikubwa katika mashindano hayo ilikuwa mpira wa miguu kwa wasichana ambapo watoto hao wa kike waliweza kuonyesha kuwa nao wanaweza kucheza michezo ya wanaume. Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ilioneshana kazi na Wilaya ya Karagwe na Bukoba kucharazwa bao 2-1.
Changamoto; Vyama vya michezo ambavyo vina wajibu na kazi ya kubaini kuinua na kukuza vipaji katika mkoa wa Kagera havikuweza kufika katika viwanja vya michezo hiyo na kushudia vipaji vinavyochipuki kwa ajili ya kukuzwa. Viongozi wanatakiwa kurudi nyuma na kuona fursa kama hizi ili mkoa uwe na vipaji vipya.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013


Next Post Previous Post
Bukobawadau