Bukobawadau

HABARI MBALIMBALI KWA MKUTASARI

Mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 67 jela wakiwemo raia wawili wa Kenya na mwanamke mmoja mtanzania baada ya kupatikana na hatia ya kula njama na kupora shilingi million 239 katika benki ya NMB tawi la Mwanga, Kilimanjaro.* * * *Uporaji huo ulifanyika julai 11,2007 ambapo watu hao waliiba bunduki aina ya Sub machine gun (SMG) mali ya Jeshi la Polisi nchini, ikiwemo kuuawa kwa askari Polisi Ex- PC Michael Milanzi aliyekuwa lindo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko
Hii haijawahai kutokea, watu kujaa hadi wengine kukosa nafasi ya kuingia ndani na kurudi nyumbani, ndiyo kilichotokea kwenye show ya Lady hapo jana
Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi. Katika hukumu iliyosomwa leo jioni, mahakama imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye uongozi.
Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akiwalaki Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead na Makamu Mwenyekiti wa POL Tayseer Khalid (mwanaume mwenye miwani) Khalid na ujumbe wake walipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, waliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wanne Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.
 Mwanamuziki Jady Jay Dee akionyesha umahiri wake wa kulishambilia jukwaa wakati wa show yake ya kutimiza miaka 13 katika Muziki iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali

Matukio mbali mbali katika show ya Lady Jay Dee Kutimiza Miaka 13 ya Muziki ndani ya kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar


Ilikuwa ni shangwe tupu wakati wa show hiyo
Credit Michuzi Blog
Next Post Previous Post
Bukobawadau