Bukobawadau

KAMACHUMU LEO SEPTEMBA 17,2013

Hapa ni round about mjini kamachumu kuelekea hospital ya Ndolage.
Hapa Camera yetu ikiangaza kwenye mji wa Kamachumu,Mji wenye hekaheka nyingi,wadau wengi ni watata sana,Mji huu ndiyo chimbuko la maaskofu wakubwa na maarufu tukianza na Askofu Mushemba wa KKKT  pia hapa anazaliwa Cardinal wa kwanza wa Afrika Cardinal Laurean Rugambwa,pia Askofu msaidizi Titus Joseph Mdoe wa Jimbo kuu la Dar es Salaam wa eneo jirani la kijiji cha Muutwe na Baba ni Mzaliwa wa kijiji cha Katoma- Kamachumu
Watu maarufu walitokea hapo yupo  
Charles Mwijage Mbunge wa eneo hili lililopo Muleba Kaskazini.
 Anthony Rugangila,Kalinjuma,na Ntonini,Haji Hamad,Byabusha,Mzee Songoro aka Karasha,familia ya Bukenya alikadhalika Zakalia Mugyabuso Petro Nshange aka (kibunda) na Christopha Ngaiza wote ni marehemu
Majemedali wengi kama Prof Lwakabamba, bora Imani,Haji Bilunduru na Haji Kabalala,Marehemu Mzee Kabea na Haji Hamad nitakua sijatenda haki nisipo mkumbuka Bandeko na familia nzima ya akina Fresh. 
Pia ipofamilia ya al-squar ndio akina mawingu ,Adara na wadau wengine wengi hii ni kwa mkutasari tu!!!
Kwa sasa wapo akina Hamed Kiwanuka , Veda Rugabela,Mdau Myaga , Mzee Thadeo Iluganyuma na Mdau Sued ukanda wa Rutabo akiwepo Mzee Nestory Kato, mdau Chamisili na mwalimu Mastura
Hii ni kwa uzoefu  wa kimazingira wa Blogger wenu Mc Baraka
Hapa ni Soko kuu Mjini Kamachumu,baada ya zao la kahawa kudorora mkoani Kagera humu sasa kuna changamoto ya ugonjwa wa mnyauko unaochukua kasi kubwa mjini Kamachumu
Shamba safi la migomba nyimbani kwa Mzee Mwandiki, kijijini Kamachumu
 Uwanja wa mpira uliopo shule ya msingi Bulembo Kamachumu.


Kuelekea kijiji cha bulembo  ndani ya kata ya Kamachumu

Wadau wakicheck na Camera yetu

Msikiti maarufu wa dhuhuri  uliopo kwa Kabea Mjini Kamachumu.
Taswira mjini kamachumu
Pichani ni Mdau Mr Kamu wa kijiji cha bulembo kamachumu, yeye ni mtaalamu wa kuunga mifupa kwa tiba mbadala ya mitishamba 
akiongea na Bukoba wadau Mr Kamu alifafanua kuwa wagonjwa wengi anaowapokea ni wale waliolazwa zwa na madaktari kuwa wanapaswa kukatwa viungo vyao ambao wakifika kwake na kutibiwa wanapona ambapo matokeo ya tiba hiyo huanza kuonekana baada ya wiki moja mpaka mwezi mmoja kutokana na umri na tatizo la mgonjwa.(Ni machache kuhusiana na huyu 'kayunga magufa' unaweza kuwasiliana nae kupitia 0753 231057)
BUKOBAWADAU

Next Post Previous Post
Bukobawadau