Mahakama ya Wilaya ya Bukoba leo tarehe 11
Mahakama ya Wilaya ya Bukoba leo tarehe 11/09/2013
imemhukumu Kifungo cha Miaka 30 mtu mmoja anayeitwa BAGAICHWAKI S/0 MATHAYO
Umri miaka 40 kwa kosa la kubaka kinyume na kifungu cha 130(2)(e) na 131(1) cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu [Sura 16 Marejeo 2002]. Katika kesi ya jinai Na. na
33/2013.
Maelezo ya Shtaka: Mshtakiwa mnamo Tarehe 18 Mwezi
Aprili Mwaka 2013 maeneo ya Nyamkazi katika Manispaa ya Bukoba Mkoa wa Kagera,
alifanya mapenzi na msichana xxxx ambaye ni msichana mwenye umri wa miaka 15.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba
Charles Uiso aliridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi wa
upande wa mashtaka wakiongozwa na Wakili wa Serikali Chema Maswi Mbena, ikiwa
ni pamoja na mhanga mwenyewe ambaye alieleza jinsi alivyofanya mapenzi na
mshtakiwa katika chumba cha mshtakiwa tarehe 18/04/2013, ambapo wakiendelea
kufanya kitendo hicho ndipo walipotokea majirani pamoja na mzazi wa msichana
huyo ambao walimuona akiingia nyumbani kwa mshtakiwa. Mahakama pia ilipokea
kielelezo cha hati ya matibabu (PF.3) kilichotolewa na mhanga (victim).
Utetezi:Mahakama haikuridhika na utetezi wa mshtakiwa
kuwa alibambikiziwa kesi hiyo kwakuwa alikuwa anamdai sh. 50,000/= baba wa
Mhanga ambapo Mahakama ilisema kuwa utetezi huo ni wa kutunga “afterthought”
kwani alipopewa nafasi ya kumuuliza maswali baba wa mhanga hakuuliza kuhusu
kiasi hicho cha pesa anachomdai.
Uamuzi:Mahakama iliridhika kuwa upande wa mashtaka
umethibitisha shtaka bila kuacha shaka lolote na hivyo ikamtia hatiani mshtakiwa.
Kumbukumbu za nyuma za uhalifu za Mshtakiwa:Upande wa
mashtaka haukuwa na kumbukumbu zozote za uhalifu za mshtakiwa hata hivyo
uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwani tabia ya watu wazima
wenye umri mkubwa kama mshtakiwa imekuwa sugu katika jamii na hivyo adhabu kali
haina budi kutolewa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hizo.
Sababu za Shufaa (Mitigation): Mshtakiwa hakusema lolote
juu ya kuiomba mahakama impunguzie adhabu
Kifungo: Miaka 30