TASWIRA MAKAMUZI YA SAIDA KAROLI NDANI YA CLUB LINAS BUKOBA USIKU WA JANA.
Msanii mkongwe wa nyimbo za asili ya Kihaya nchini mwenye sauti ya aina yake,mkali wa kughani na kipaza sawa na WHITNEY HOUSTON nasema hivyo kwa sababu ukiisikiliza I Will Always Love You ya Whitney na ukasikiliza mistari ya Saida Karoli kama 'Nkaba ninja kiyanja' AU Khalid na Philmon walipendana' hakika utakubaliana na mimi katika hiki nikisemacho
Tamasha la Saida Karoli limeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ndani ya Kiota cha Lina's Night Club,Pamoja na mshkeri uliojitokeza mapema wakati wa matangazo ya barabarani kufuatia gari la PA kupata ajali likiwa eneo la Kashura na kumnusuru Saida huku mwenzake Papaa Kishaju akipata majeraha kidogo na kama kawaida ya buhaya uvumi ukatanda kupita kiasi lengo likiwa lile lile tu 'KUTENDELANA' na wapo waliodai kuwa Onyesho hilo halipo kumbe ndivyo sivyo.
Mwanzo wa shughuli ile mapema tu,tayari watu wanapandisha midadi katika kujivunia # kikwetu kwetu kama anavyo onekana Mdau William Rutta wa kampuni ya Utalii ya Kiroyera.
Hivi ndivyo mambo yanavyokuwa, mtu anapo pata hisia...
Msanii Saida Karoli na mkurugenzi VMA(VISION MUSIC AMBASSADOR) Miss Matrida Leopord
Picha ya pamoja wasanii wa VMA
Show mbalimbali zikiendelea
Home kutoka Muleba akifanya yake, ni msanii Bk Sande.
Msanii BK Sande akiwajibika jukwaani
Mwanadada Maua Ramadhani akifuatilia show.
Maelfu ya wadau ndani ya kisima cha burudani
Afisa utamaduni manispaa ya Bukoba Ndg Rugehiyamu kulia katika picha ya pamoja na muandaaji wa tamasha hili mkuugenzi wa Tivol Studio wa jijini Mwanza.
Kaka Mkubwa kushoto na Mdau William Rutta.
Uwezo na tofauti kubwa kati ya Msanii Saida Karoli na wasanii wengine katika kupiga ngoma na uimbaji
Kwa raha zao mashabiki wakijiachia.
Naaam!
Kutoka kushoto ni Mdau Jane Zachwa, Mkubwa Papaa Muganyizi na Mwanalibeneke Jamal Kalumuna .