Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, ameachia ngazi
Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, ameachia ngazi/kiti hicho alichokuwa amekishikilia kwa miaka kadhaa huku nyuma yake kukiwa na shinikizo la kumtaka aondoke kutokana na kuporomoka kwa kiwango cha elimu nchini katika miaka ya karibuni.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Baraza hilo, Prof Rwekaza Mukandala, Ndalichako ameondoka NECTA na nafasi yake itakuwa ikikaimiwa na Dr Charles Msonde aliyekuwa msaidizi wake. Akifafanua kuhusu kuondoka huko kwa Dr. Ndalichako, Prof. Mukandala, amesema kwamba Dr Ndalichako ameanza likizo ya utafiti (Sabbatical leave) ya mwaka mmoja kuanzia Oktoba mwaka huu hadi Septemba 2014.
Taarifa ya mwenyekiti huyo haijafafanua wala kuhusisha kuondoka kwa Dr. Ndalichako na taarifa za kuwepo shinikizo la kisiasa na kijamii lililokuwa likimzonga kutokana na matokeo mabaya ya mitihani sanjari na kuporomoka kwa elimu nchini.
www.jukwaahuru.com