Bukobawadau

VURUGU KUBWA ZAZUKA JIJINI MBEYA,WAFANYABIASHARA WAGOMEA MASHINE ZA TRA.

Mataili yakichomwa moto barabarani.
 Polisi wakiwa katika ulinzi mkali
 Wafanya biashara wakiwa uwanjani kungoja kusikiliza nini hatma yao
 Mawe yakiwa yamepangwa kuzuia magari yasiende kokote
 Maduka yote yakiwa yamefungwa eneo la mwanjelwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA
  Vijana hawa wakiwa wana nawa uso baada ya Bomu la machozi kuwapitia

HALI IMEREJEA KUWA MBAYA TENA JIJINI MBEYA, MAENEO YA MWANJELWA HAPA.... NI MABOMU KWAKWENDA MBELE SASA...
Baada ya vurugu za asubuhi, mchana kulitolewa tangazo kuwa kungekuwa na mkutano wa wafanyibiashara eneo la mbele ya soko jipya la mwanjelwa, na ikawa hivyo ilipofika majira ya saa nane watu wakawa wamejikusanya hapo kwa ajili ya mkutano. Hata hivyo, likazuka suala la kuwa waliokuwa wamekamatwa asubuhi waachiwe ndipo mkutano uendelee.

Waliokuwa kituo cha Mwanjelwa, waliachiwa, ikaja waliokuwa Central, ambao ilikuwa wakaachiwe nasikia, lakini wananchi wakadhania wanapigwa changa la macho, sasa wakaanza maandamano kuelekea Central kuhakikisha wenzao wanaachiwa....kilichoendelea.... ni mtafutano hivi sasa kila mahali.

Ndani ya muda wa dakika 10, tayari zaidi ya mabomu 50 ya machozi yameshapigwa. Inawezekana Polisi wakawa wanaona kuwa hatua hii itatuliza mambo, lakini kwa mtazamo wangu na uzoefu wa watu wa jiji hili, naona kama hali ndio itazidi kuwa mbaya zaidi...

Pichani, ni wananchi wakionyesha mshikamano wao kukataa kumsikiliza yeyote hadi wenzao waachiwe, na nyingine ni Polisi wakijipanga kuanza kufanya kazi yao - Picha zote ni kwa hisani ya mdau Stanslaus Lambat
Next Post Previous Post
Bukobawadau