Bukobawadau

TAMASHA LA UJASIRIAMALI MWANZA, ELIMU, BURUDANI MWANZO MWISHO

Mwanamuziki Fid Q akizikonga nyoyo za mashabiki wa Mwanza waliohudhuria tamasha la ujasiriamali jana.

Mheshimiwa Sugu akitoa burudani kwa wakazi wa Mwanza ndani ya CCM Kirumba.

Young Killer akiingia kwa mbwembwe uwanjani.

Young Killer akifanya makamuzi ya nguvu ndani ya CCM Kirumba jana.

H-Baba akikamua katika Tamasha kubwa la Ujasiriamali lililofikia mwisho jana.

...H-baba akiwasalimia mashabiki wake.

Msanii Jitaman akitumbuiza.

Mkurugenzi wa Global Publishers na Street University, Eric Shigongo akitoa elimu ya ujasiriamali kwa wakazi wa Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Eric Shigongo akimsikiliza mmoja wa watu waliofanikiwa kupitia mafundisho yake ya ujasiriamali.

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Mheshimiwa Joseph Mbilinyi 'Sugu', akiwafundisha wananchi wa Mwanza.

Watu waliojaa ndani ya CCM Kirumba kufuatilia tamasha hilo..

Askari wakidumisha ulinzi uwanjani hapo.Nyomi iliyohudhuria tamasha hilo jana.

Joseph Mbilinyi 'Sugu' akipozi na H-Baba.

Tamasha kubwa la Ujasiriamali lililofikia tamati jana jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza lilitawaliwa na elimu pamoja na burudani kali kutoka kwa wasanii Fid Q, H-Baba, Young Killer na Jitta Man. Kwa upande wa injili, burudani hizo ziliongozwa na Martha Mwaipaja na Emmanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji. Walimu wa ujasiriamali nchini, Eric Shigongo na James Mwang'amba wakiwa sambamba na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Mhe. Joseph Mbilinyi 'Sugu' walitoa elimu ya ujasiriamali kwa wakazi wa Mwanza na kuwaacha wakiwa wameiva kwenye masuala hayo.

(PICHA: CHANDE ABALLAH NA DENIS MTIMA / GPL, MWANZA)

Next Post Previous Post
Bukobawadau