Bukobawadau

UZINDUZI MIRADI YA DASIP KIKUKWE

Na  Mutayoba Arbogast,Missenyi
Serikali za vijiji zimetakiwa kutumia sheria ndogo ndogo kuhakikisha miradi mbalimbali ya kilimo na ufugaji inayoendeshwa na halmashauri za wilaya chini ya mpango wa DASIP,inatimiza matarajio.
Wito huo umetolewa 19/12/2013 na Bibi Anagrace Kagaruki,ambaye ni afisa kilimo na mratibu wa vikundi vya DASIP katika wilaya ya Missenyi wakati wa hafla ya uzinduzi wa miradi ya DASIP iliyokwisha kamilika katika kijiji cha Kikukwe,kata ya Kanyigo wilayani Missenyi.
Afisa huyo amekemea tabia ya baadhi ya vijiji kuendelea kuruhusu uuzwaji holela wa mazao ya vyakula wakati tayari kuna masoko ya DASIP vijijini humo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Samweli Bashweka akiitabulisha miradi hiyo ambayo imezinduliwa kijijini humo ni ujenzi wa soko lililogharim sh milioni 20,DASIP ikiwezesha sh milioni 16 na jamii ikichangia sh milioni nne,kibanio kwa ajili ya huduma ya mifugo kikiwa kimegharimu zaidi ya sh milioni  saba nalaki nane DASIP ikiwezesha zaidi y ash milioni sita na laki tano na jamii zaidi ya shmilioni moja na laki tatu.Mradi mwingine ni wa mashine ya kusaga wenye thamani ya sh milioni saba.
Mwenyekiti wa kijiji hicho ameitangaza  Alhamisi ya kila wiki kuwa siku ya gulio kijijini humo.
Kuzinduliwa kwa miradi hiyo  kumeenda sambamba na tathmini ya miradi hiyo ili kupima ufanisi. Watatmini washauri kutoka kampuni ya EMCO RESEARCH GROUP LTD ya jijini  Dar es salaam wameendesha zoezi la kuwahoji kwa kujaza madodoso viongozi wa kijiji na wasimamizi wa miradi ya DASIP kijijini,na wanavikundi.
MWISHO
Next Post Previous Post
Bukobawadau