Bukobawadau

NGARA YAJIPANGA KUFAULISHA KWA KIWANGO KIKUBWA KATIKA BRN

 Mwalimu mkuu shule ya msingi Ntanga Mwl. Sendabaye Justus akikabidhiwa kinyago baada ya shule yake kupata ufaulu wa wastani wa 16% matokeo ya darasa la saba mwaka jana
Katibu Tawala wilayani Ngara Ndugu Vedastus Tibaijuka akikabidhi kinyako kwa Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura
 Picha  zote na habari kwa hisani ya ya Shaaban Nassibu Ndyamukama kutoka Ngara.
 Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura akipokea kinyago kutoka kwa katibu Tawala wilayani Ngara Vedastus Tibaijuka baada ya kata yake na tarafa kupata ufaulu duni wa 39% kwa kata & 52% kwa tarafa
 Pichani ni Mwalimu mkuu shule ya msingi Ntanga Mwl. Sendabaye Justus
 
IDARA ya elimu ya Msingi wilayani Ngara Mkoani Kagera  imejiwekea mikakati ya  kukutekeleza malengo ya kitaifa ya Big Results Now kwa 70% baada ya kupata walimu wapya 139  mwaka huu watakaoungana na 1543 waliokuwepo  awali.
Katika utekelezaji huo  wazazi , walimu na wanafunzi katika shule , na kata zilizoko tarafa ya Murusagamba wilayani  humo wametakiwa kuongeza juhudi za kuinua kiwango cha taaluma  katika tarafa hiyo ili kuingia katika wa malengo hayo
Ofisa elimu idara ya msingi wilayani Ngara Simon Mumbee alisema hayo juzi kwenye  maadhimisho ya wiki ya elimu wilayani humo na kudai  tarafa hiyo iko nyuma kitaaluma katika shule zake 13 zilizoko  kata ya Muganza na Mursagamba
Mumbee alisema tarafa hiyo imekuwa ya mwisho katika ufaulu wa mitihani ya darasa la saba mwaka jana kwa kupata 52% ya wastani wa ushindi kitaifa ambao ni 60% na kata ya murusagamba ilikuwa ya mwisho kiwilaya kwa  ufaulu wa 39%  
Alisema kuwa katika wastani wa ufaulu kitaifa mwaka jana wa 60% tarafa ya Kanazi ilifaulisha kwa wastani wa 76%,Rulenge 71% na Nyamiaga 70% na kwamba wilaya hiyo ilikuwa na wategemewa wa kufanya mtihani 3913 katika shule 118.
Alifafanua kuwa mwaka jana wilaya hiyo  ilikuwa na watahiniwa  waliofanya mtihani walikuwa 3861  wavulana 1790 na wasichana 2071 sawana 99% ambao walifaulu ni 2683 wavulana  1311 wasichana 1372 sawa na wastani wa 69.5%.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na ufaulu huo bado katika shule 903 zilizoko Mkoani Kagera  shule ya msingi Ntanga kata ya Murusagamba wilayani humo ilikuwa ya mwisho  kimkoa kwa kuwa na wastani wa 16%
“Napenda kuwatia moyo uongozi wa tarafa kata na shule wakiwemo wazai na wanafunzi wenyewe kuoneza juhudi ili kuweza kufanya vizuri kwa matokeo ya mitihani mwaka huu”Alisema Mumbee
Aliongeza kuwa idara ya msingi wilayani humo  ina jumla ya shule za msingi 118 kati ya hizo shule nne ni za binafsi  na nyingine za serikali zote zinao   wanafunzi wa elimu ya awali 12188 kati yao wavulana ni  5292 na wasichana ni 5356.
Pia  shule hizo zinawanafunzi wa darasa la kwanza hadi la saba wapatao 73978 kati yao 36758 ni wavulana na 37220 ni wasichana  ambapo  wanafunzi wa elimu ya MEMKWA ni 2200 kati yao wavulana ni 1355 na wasichana 845.
Kwa upande wake afisa elimu Taaluma Fidelis  Apolinari alizitaja shule zilizofanya vizuri katika  mtihani  na kutuzwa zawadi na vyeti vya taaluma bora  kuwa ni  Prince (English Medium) ya kwanza kiwilaya, kimkoa na ilikuwa ya saba kitaifa
Alitaja pia shule ya Mwanga (English Medium) ambayo ilikuwa ya pili kiwilaya  ya tano kimkoa na 14 Kitaifa huku  Rhec (English Medium) ilikuwa  ya tatu kiwilaya na saba  kimkoa ambapo kitaifa ni ya 17 kati ya shule
Alisema shule nyingine ambazo ni shule za serikali zilizofanya vema ni  Murgwanza Ngara mjini , Murukukumbo, Kabalenzi , Mubinyange, Nakatunga na Ntungamo ambapo kata ya kwanza ni Ngara mjini yenye ufaulu wa wastani (98%)
“Shule zenye taaluma hafifu ni Ntanga ,Murugunga ,Rusengo Kabaheshi
Kirushya, Nyankende ,Ntobeye, Kasulo, Kanyinya na Kabulanzwili”. Alisema
Kwenye kilele cha wiki ya elimu iliyopambwa kwa kauli mbiu isemayo Elimu bora Kuboresha Mtanzania katika wilaya hiyo   kata tarafa na shule ilizokuwa za mwisho zilizawadiwa vinyago na cheti chenye taaluma hafifu.  
Pamoja na taarifa hiyo Katibu Tawala Vedastus Tibaijuka kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu katika hotuba yake aliwataka walimu kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kuboreshewa mazingira ya kufundishia
Tibaijuka alidai walimu  katika wilaya hiyo wanahitaji kuwa na nyumba za kuishi katika shule zao kupata zana bora za kufundishia na kupata mafunzo elekezi katika kuwaongezea ujuzi na maarifa kulingana na mabadiliko ya teknolojia.
Alitaja baadhi ya changamoto katika utoaji wa taaluma kuwa ni ulevi wa walimu na kujihusisha na biashara ya bodaboda saa za kazi , mikopo mingi katika taasisi za kifedha na hatimaye kushindwa kuwajibika kiutumishi na kifamilia.
 MWISHO.
Next Post Previous Post
Bukobawadau