Bukobawadau

JIONEE!!YALIOJILI HARUSI EDISON MHAGAMA NA BEATRICE MARWA MAY 18,2014

 Bwana Edson Mhagama akidondosha wino wa kukiri kwamba alimaanisha alichokisema mara baada Ibada ya ndoa iliyokuwa ikiendelea katika kanisa la Anglikan lililopo barabara ya Uganda ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba
 Mchungaji Bililiza wa Kanisa la Anglikan Bukoba akifuatilia tukio la Bi Harusi, Bi Beatrice Marwa kusaini cheti cha ndoa, kitendo kinacho mpa na bashasha Bwana Edison Mhagama
 Sasa ni Bwana na Bibi Edson Mhagama.Mwanzoni Ilikuwa kama utani hivi jamaa alipotunyooshea maelezo kwamba anataka kufunga ndoa Rasmi! Watu tukachukulia simple tukajua kama kawaida jamaa hupenda utani. Mara he! Tarehe 18 May 2014 yakatimia kweli. Mdau Edison akaamua kuliaga chama la makapera na kupanda gari isiyokuwa na gear ya reverse. Akafunga pingu za maisha na Bi Beatrice Marwa . Wakaamua kuishi pamoja for the rest of their life.
 Furaha ya ndoa jamani kusoma hamjui. Hata picha hamwoni? She is mine alimalizia Mdau Edison Mhagama
 Mr & Mrs Edson Mhagama katika picha ya pozi pande za mchangani,mara baada ya tukio hili inafuatiwa kufatiwa na sherehe kubwa iliyokusanya watu kibwena iliyofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Club uliopo maeneo ya fukwe za Ziwa Victoria.
 Maharusi wakiingia ukumbini,wakiwa sambamba na wapambe wao
Maharusi wakikata utepe kuingia Ukumbini
Muonekano wa Keki
Mdau Didas Fridolin Kambona akimsimamia Bwana Edison Mhagama  na mkewe Beatrice Marwa wakikata Keki  wakati wa tafrija ya ndoa yao iliyofanyika usiku wa jumamosi  kwenye ukumbi wa Bukoba Club
 Wakilishana keki
 Maharusi wetu wanavyo meremeta.
 Kitendo cha Marusi wetu kupeleka zawadi kwa wazazi 
 Bi Beatrice akikabidhi zawadi kwa wazazi wa Bwana Harusi
 Wageni waalikwa ukumbini.
 Anaonekana Bi Anitha (Mrs Divo Lugaibula).
 Mdau Mgeni mualikwa akiendelea ku 'kick' kupitia Android yake.
Matukio ya harusi ya Bwana na Bibi Beatrice Marwa.
Wadau wakisikilizia maneno kutoka kwa washereheshaji wetu kwa usiku huu.
 Shughuli hii imeongozwa na Ma Mcee wawili wenye uwezo sawa,na wenye kufanana.
 Mc na 1 ni Mc TUMA,Mc mwenye uwezo wa kufanya shughuli yako kulingana na matakwa yako
 Mc. namba 2, MC mashuhuri kwa Corporate Events\Weddings\Send Off parties na majumuiko mbalimbali yenye hadhi yake,mdau msomaji kama unataka msema chochote mwenye staha, msomi na anayechangamsha shughuli basi wasiliana nasi.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ndugu Subira akitoa kile kamati ilichokiandaa kama zawadi kwa Bwana na Bibi Edison Mhagama
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi akitoa utambulisho kwa wanakamati.
 Zoezi zima la utambulisho kwa wanakamati likiendelea
 Mr.China mmoja wa wanakati katika utambulisho. 
 Kama ulikuwa ufahamu  huyu ndiye MC Jerry, mmoja wa ma MC mashuhuri na makini wa hapa Bk, kama anavyo onekana akitoa bonge la show wakati wa kuwajibika kwake.
 Moja ya meza iliyo onekana kutulia na kupendeza ile mbayaa!!
 Muonekano wa wanakati  katika picha na Maharusi wetu
 Mara baada ya Kupokea Cheki
Bwana na Bibi Edson Mhagama.
 Kamati nzima ya maandalizi ya harusi hii wakiwa Sambamba na Bwana  na Bibi Edson Mhagama
Wapambe wa maharusi wakifanya kulindana kidogo
Mdau Amani Kabuga akipata msosi


 Zoezi la kupata msosi likiendelea
 Maharushi na mtoto wao wakiwa wenye nyuso za furaha na bashasha tele.


Next Post Previous Post
Bukobawadau