Bukobawadau

KAMACHUMU YAPENDEKEZWA WILAYA MPYA

 MKUU wa Wilaya (DC) ya Muleba, mkoani Kagera, Lembris Kipuyo
MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera jana wameazimia kuigawanya wilaya hiyo kuwa wilaya mbili ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo ya wananchi ili kujipatia huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na utawala wa karibu kwa baadhi ya kata za mbali na Muleba.
Katibu wa madiwani wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo Fortunatus Wazia amesema wilaya hiyo kijografia ni kubwa kwa kuwa na kata 43 na vijiji zaidi ya 160 ambapo upatikanaji wa huduma za jamii huchelewa.
 Wazia  amesema katika kuigawa wilaya hiyo kamati ya madiwani wa CCM inapendekeza ramani iliyochorwa  kugawa wilaya hiyo katika majimbo ya uchaguzi mipaka hiyo  itumike kwa wilaya  mpya inayopendekezwa.
 Aidha alisema kuwa kisiwa cha Goziba ambacho kiko mpakani mwa mkoa wa kagera na mwanza kikimilikiwa na wilaya ya Muleba kiendelee kuwa mkoani kagera badala ya kupelekwa wilaya ya Ukerewe  mkoani Mwanza.
Kauli hiyo imeungwa mkono na kambi ya upinzani chini ya msemaji wake diwani wa kata ya Kishanda  Alfred Pastory (CUF) ambaye alisema kwa kuzingatia maoni ya wataalamu na jografia ya wilaya makao makuu ya wilaya mpya pawe kata ya Izigo.
 Alitaja sababu za kupendekeza kata hiyo kuwa makao makuu ya wilaya kuwa ni kuwepo maeneo mapana ya kujenga ofisi na miundombinu nyingine kuliko kupeleka makao makuu kata ya Kamachumu panapohitaji  kutoa fidia ya ardhi 
 Pichani ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Muleba Alhaji Swaibu
 Pamoja na maoni hayo baadhi ya madiwani walivutana katika kupendekeza makao makuu ya wilaya  diwani wa kata ya Kashasha Jonathan Manwah alipendekeza Kamachumu iwe jina la wilaya mpya na makao makuu kwa kuzingati maoni ya wataalamu pawe izigo kauli iliyoungwa mkono na madiwani walio wengi
  Hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Alhaji Swaibu Mfuruki na Mkuu wa wilaya ya Muleba Lambris Kipuyo waliwataka madiwani hao kuhakikisha wanashirikiana na wananchi pamoja na serikali kuhimiza a maendeleo hasa upatikanaji wa huduma za jamii
 MULEBA: Na Shaaban Ndyamukama

Next Post Previous Post
Bukobawadau