Bukobawadau

MREMBO MWINGINE ANASWA HONG KONG!

Mrembo mwingine wa Kitanzania almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' anaye jishughulisha na  muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi nchini China.
HUKU modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo. kwa sasa Wabongo wanaokwenda au wanaokaa China wanaishi kama digidigi kwani wamefikia hatua ya kutoonesha pasipoti zao na hata wengine wanadiriki kukataa uraia wao kwa kuwa Wabongo ndiyo wanasakwa kwa wingi. “Sasa hivi jamaa wakisikia huyo ni Mtanzania wanamfuatilia sana kwani ndiyo wenye sifa ya uingizaji wa dawa za kulevya nchini China,” kilisema chanzo hicho na kuongeza 
 
 Winnie Mandela' wa muziki wa kizazi kipya Bongo akiwa chini ya ulinzi mkali China.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa kwa msako maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa Hong Kong, China.
JUX, PETIT MAN WAPATA WAKATI MGUMU
Kwa mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva, Juma Khaleed ‘Jux Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa madawa ya kulevya nchini China
 
MADAI YA KUBEBA UNGA
Ilidaiwa kwamba Winnie alijikuta mikononi mwa askari wa China akidaiwa kubeba mzigo wa unga tumboni hivyo kukamatwa na kutembezwa mitaani kuelekea kituo cha polisi.

APITA VIZUIZI, AKAMATWA
Ilisemekana kwamba Winnie ambaye ni msichana wa mjini Dar, alifanikiwa kupita vizuizi vyote lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nchini humo ndipo akajikuta akikamatwa na kutembezwa mtaani kama mhalifu wa kivita.

“Unaambiwa ilikuwa kama vita kwani polisi wa China huwa wana silaha za kutisha sana. Unajua Winnie alikamatwa kwenye mitaa ambayo kuna Wabongo wengi hapa Hong Kong,” kilisema chanzo chetu kutoka Hong Kong.
Ilidaiwa kwamba askari hao walipokea agizo maalum kutoka kwenye kitengo cha kudhibititi madawa ya kulevya nchini humo kwani kwa sasa nchi hiyo imechafuka kwa uingizwaji wa madawa ya kulevya, jambo ambalo limeifanya serikali ya China ifanye oparesheni kubwa ya kuhakikisha wanatokomeza wimbi hilo.
KWA WABONGO CHINA
Chanzo chetu kilisema kwamba kwa sasa Wabongo wanaokwenda au wanaokaa China wanaishi kama digidigi kwani wamefikia hatua ya kutoonesha pasipoti  zao na hata wengine wanadiriki kukataa uraia wao kwa kuwa Wabongo ndiyo wanasakwa kwa wingi.

“Sasa hivi jamaa wakisikia huyo ni Mtanzania wanamfuatilia sana kwani ndiyo wenye sifa ya uingizaji wa dawa za kulevya nchini China,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
KAMA HUAMINI MUULIZE JUX AU PETIT MAN
“Hicho ndicho kilichomtokea Winnie. Nakwambia Wabongo wanazidi kukamatwa na madawa ya kulevya. Yaani ni aibu, huwezi kuamini.

“Wabongo wengi sana wamekamatwa Hong Kong na wengine familia zao Bongo hazijui.
“Kama Watanzania hawaamini wawaulize Jux na Petit Man ambao walishuhudia mtiti mwanzo mwisho.”

BALOZI WA TANZANIA CHINA
Ili kupata undani na idadi ya Watanzania wanaokamatwa kwa ishu za madawa ya kulevya nchini China, gazeti hili lilimtafuta Balozi wa Tanzania China, Luteni General Abraham Shimbo ambapo simu yake ya ofisini iliita bila kupokelewa.

Wakati Jack Patrick akisubiri kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine mwezi ujao, ripoti zinaonesha kwamba wapo Watanzania wengi waliofungwa na wengine kunyongwa kwa msala wa madawa ya kulevya.

Next Post Previous Post
Bukobawadau