Bukobawadau

UZUNGUNI(MIEMBENI 2-1 USWAHILINI (BILELE)

 Uwanjani Kaitaba timu ya Miembeni maarufu kama watoto wa Uzunguni wamefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali, kwa kuwatoa Wajanja wa town Uswahili Bilele kwa mabao 2-1 kwenye mcheze wa nusu fainali ya michuano ya Kagasheki Cup 2014 iliyochezwa Jioni ya leo July 30,2014
Mashabiki Uwanjani Kaitaba wakishuhudia #‎Kagasheki‬ Cup ni ligi yenye msisimko /upinzani na kupendwa sana na Wakazi wa Mji wa Bukoba.


 Bilele wamekuwa wa kwanza kupata bao kwa njia ya penati ,na miembeni wanazinduka na kuonyesha utulivu pia kutawala kiungo huku wakicheza pasi fupi fupi na kusawazisha bao 1-1 ndani ya dakika 90 za mchezo.
Kipa wa Miembeni akiwa amelala chini baada ya kufanyiwa Umjini.
Kipa wa membeni akisikilizia maumivu.
 Bao la pili la Watoto wa Uzunguni Miembeni limepatikana ndani ya dakika 30 za muda wa ziada (EXTRA TIME)
 # Gumzo kubwa mtaani ni USHINDI wa miembeni huku wakiwa pungufu baada ya wachezaji wawili kupewa kadi nyekundu.'Noooomah SANA!!!
 Dj Sley wa 88.5 Kasibante Fm Radio akishow love na Mr &Mr Fidel pichani
 Mdau Ayaz na Mdau Nuru wakifuatilia soka.
 Taflani uwanjani.
 Bango la Timu ya Bilele maarufu kama wa 'Hapa hapa'Km 0.
Mwamuzi anatoa kadi ya nyekundu kwa mchezaji wa Miembeni
Kushoto ni Shangwe za shabiki wa Miembeni Kijana Obeid 'Oda Man'pichani kushoto huku akiwavunja mbavu Ndugu Kagunguna na Mdau maarufu kwa jina la matunda pichani kulia.
Baada ya Mechi anaonekana Ndugu al Amin Abdul akijaribu kuwaokoa waamuzi wa Mchezo huu baada ya kutaka kutembezewa kichapo.


 Sehemu ya mashabiki wa miembeni wakishangilia ushindi
 Akiongoe na Bukobawadau Entertainment Media Kiongozi wa Miembeni'Super Star' Mwinyi Kheeir pichani( kulia)ambaye kwa sasa Jina lake linamake headline baada ya kuwaondoa kijemedali Wana wa Kashai katika mchezo wa robo wa fainali na leo kawabwaga Vijana wa Mjini Maarufu kama WA HAPA HAPA Km 0 Uswahilini Bilele amesema;'Kilichobaki sasa wakaungane na wenzao katika rufaa'

Next Post Previous Post
Bukobawadau