Bukobawadau

SERENGETI FIESTA 2014 SAMBAZA UPENDO.......NI SHEEEEEDAH!!

Tamasha la Serengeti Fiesta kwa mara ya kwanza ndani ya Mji wa Bukoba linatarajiwa kurindima siku ya Ijumaa Aug 15,ndani ya Uwanja wa Kaitaba,Tayari sehemu ya wadau wamewasili mjini hapa usiku huu ikiwa ni pamoja na Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja.
.Gari la kurusha matangazo likiwa limeegesha maeneo ya Kiroyera Tours.
 Baada ya Mwanza kukata utepe wa Serengeti fiesta ya mwaka huu kwa siku ya jumamosi. harakati za kusambaza upendo sasa zinahamia bukoba kwa siku ya ijumaa hii ya tarehe 15 mwezi huu, na kahama ambapo itakuwa siku ya jumapili ya tarehe 17 mwezi huu. sasa nikupe mchongo wa mastaa wako utakaoweza kuwashuhudia; Ommy Dimpoz,Young Killer,Barnaba,Madee,Jux,Ney wa Mitego,
Stamina,Mr. Blue,Recho,Linah,Super Nyota, Khadija wa Maumivu na BK sunday. 
Kumbuka, shangwe hili lote utaweza kulifaidi kwa kiingilio cha shilingi 5000 tu itakayokupa nafasi wewe mkazi wa Bukoba kupenya ndani ya Kaitaba Stadium na kwa wewe mkazi wa Kahama kujichanganya kahama stadium sehemu pekee ambapo historia ya fiesta ya kwanza itaandikiwa.
Katika hili na lile anaonekana  (Technician)Godwin Sanga
 Meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii ya Kiroyera,Ndugu  William Rutta  akionyesha furaha yake na kuwasha 'Flying Lantern'  ikiwa ni ishala ya Fiesta kwa mara ya kwanza.Mkoani Kagera
 Mdau Willy Rutta wa Kiroyera  pichani
Chinese Flying Lather inaruka angani ikiwa na moto kwa dakika 20
Macho ya wadau yakifuatilia mpaka mwisho.
  Anaonekana akipata Chai Ndugu Samadu Abdul wa Clouds Fm 88.1 Mwanza
 SERENGETI FIESTA 2014 SAMBAZA UPENDO.......NI SHEEEEEDAH!!


Next Post Previous Post
Bukobawadau