Bukobawadau

SHUKRANI KUBWA KUTOKA KWA MC BARAKA!!

Nitumie muda huu baada ya siku ya kuzaliwa kwangu Aug 23,kuwashukuruni WADAU nyote kwa kuwa sehemu muhimu ya maisha yangu.
Rafiki zangu wa fb mmefanya noma sana maana mpaka sasa nimepokea ujumbe wa kunitakia heri ya KUZALIWA kupitia wall na GROUPS kutoka kwa watu zaidi ya 600.
Watu wangu wa Twitter na Instagram nimeona mlivyofunguka kiukweli ninachoweza kusema ni kwamba ' Mwashagao' nimeamini 'maji yaweza kuwa mazito kuliko damu nyie ni marafiki wenye kujali ile mbayaa!!

Nikianza na Ndugu Zangu 'Wanyaluganda' wanaukoo wa Galiatano Sitoweza kuwataja mmoja mmoja, lakini kwa ujumla wenu mmekuwa mkishiriki sana katika maisha yangu. Siku zote natambua kuwa sina cha kuwarudishia kifananacho na wema wenu kwangu.Mungu awabarikini sana 'Waitu nimbasima mno' na ninawapendeni sana.!!
 Rafiki zangu Paul Rwechungura, Shamila Ismail,Abby Candy ,Gara B Kubwa Ashraf Lugusha Dadaa Kabendera. Ben Kataruga,Jovy Mujwa Rukambuzi ,Fuady Rugusha ,Jerome Rugemalira ,Mkurugenzi Peter Mgisha ,Linas L. Mtensa na Rahym Kabyemela ,Ninayo sababu ya kuwashukuru kipekee,Kuwa nanyi ni namna ambayo Mungu amependa na kunipa sababu ya kujivunia .
"Kwangu ku-blog kumekuwa KUISHI. Ni sehemu ya maisha na ninajiona kama mwana-FAMILIA kwenye ulimwengu huu. Nimejuana na wengi toka sehemu nyingi  na kujuana huku kunaniwezesha kushirikiana na wengi."hayo ni maneno ya Mwanalibeneke Mubelwa Bandio
Shukrani kwako Prudence KarugendoRama S. Msangi,Kajunason BLOG - Cathbert Angelo.Geofrey Adroph, Sirloom Galiatano na wanablog wenzangu, ambao sasa tumekuwa familia moja kubwa iliyoungana vyema

Nimalizie,tena kuwashukuru WADAU nyote kwa ujumla wenu,Kila kundi ni sehemu muhimu sana maishani mwangu.
Salute kwenu Ndugu nawapenda Sana!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau