BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKUU WA IDARA YA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA JIJI LA OESTENDE LA UBELGIJI
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na Mkuu Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa
Jiji la Oestende la Ubelgji Mhe. Collins Nweke (katikati). Mhe. Collins
alifika ofisini kwa Balozi Kamala kumweleza mipango ya Jiji la Oestende
kushirikiana na Tanzania. Kushoto ni Mhe. Nyamtara Mukome Mratibu wa
Masuala ya Uchumi katika Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji.