Bukobawadau

SHEREHE YA KUMPONGEZA GISSELA MONTANIUS KUMALIZA CHUO KIKUU (SHAHADA YA SHERIA)

Hakika anastahili Sifa Mwanadada Gissela R. Montanius pichani,katika sherehe ya kumpongeza kwa kumaliza Chuo Kikuu  shahada ya kwanza ya Sheria.
 Sherehe hiyo iliyoandaliwa na Mama yake Mzazi Bi Lucy Salvatory pichani kushoto imefanyika  katika  Ukumbi wa Lake Hotel Bukoba.
Mama Mzazi Bi Lucy Salvatory akionesha upendo wa dhati kwa kumlisha keki Mwanae Gissela.
Hapa Gissela anamlisha mama yake Keki
 Bibi naye analishwa tamtam katika Sherehe hiyo ndogo ya kumpongeza Mjukuu wake Gissela kwa kumaliza Chuo Kikuu  shahada ya kwanza ya Sheria.
Mama zake wadogo nao walikuwepo
 Ndugu mbalimbali wa familia ya Mzee Salvatory Kato wa Kijini Kanyiko -Bukwali wameweza kushiriki katika sherehe hiyo.
 Katika picha ya kumbukumbu,kushoto ni Ndugu Inayat Visram, mzazi mlezi wa Ms Gissela
  Pamoja na zawadi za awali alizozitoa kwa Mama yake,Kama haitoshi Gissela anaendelea kumzawadia Mama yake Ukumbini .
 Burudani ya Muziki ikichukua kasi katika sherehe ya kumpongeza Mwanadada Gissela.
Sehemu ya Waalikwa na marafiki zake Gissela wakicheza muziki kwa pamoja.
Kwa pamoja wakipata chakula na waalikwa wote ikiwa ni sherehe Maalum kumpongeza Gissela .


Next Post Previous Post
Bukobawadau