Bukobawadau

VURUGU ZA BODABODA NA POLISI BUKOBA

 POLISI  mjini Bukoba wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waendesha pikipiki maarufu kama Asecdo /bodaboda waliojikusanya kwa wingi kama ilivyo kawaida yao pale  mwenzao anapopatwa na Matatizo , Lengo la waendesha pikipiki hao ikiwa ni kumsaidia  mwenzao aliyekamatwa na Askari kwa tuhuma za kubeba Abiria bila kuvaa kofia ngumu (Helmet).
 Vurugu hiyo inadaiwa imetokana na kuchoshwa na Vitendo vya uonevu wanavyofanyiwa na Askari vya kuwakamata ata wanapokuwa hawana makosa.
 Vurugu hizo zilizotokea jioni ya jana kati ya makutano ya barabara ya Jamhuri na Kashozi jirani kabisa na Bank ya CRDB tawi la Bukoba iliyo shambuliwa kwa mawe na matofari na kundi la waendesha bodaboda hao.
Picha ya Faustin Lutta inaonyesha mwenzao huyo akiwa chini ya Ulinzi tayari kupelekwa kituoni.
Baada ya Vurugu hizo tayari waendesha bodaboda kadhaa wamekamatwa na bado wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya Vurugu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau