Bukobawadau

ZIARA YA VIONGOZI CWT NGAZI YA MKOA NA WA WILAYA YA MISSENYI KUKUTANA NA WALIMU KATA ZA KANYIGO NA KASHENYE

 Katibu kitengo cha wanawake CWT Mkoa,Lucy Tibiita akifafanua masuala ya wanawake wakati wa mkutano huo.
 Viongozi wa CWT Mkoa na  wa wilaya ya Missenyi:wa pili kutoka kushoto ni katibu mkoa,Pontian Gervase,wa nnne kutoka kushoto ni mwenyekiti mkoa ,Dauda Bilikesi,na wa pili kutoka kulia ni Katibu CWT Wilaya ya Missenyi,Livingstone William
Mwalimu Daniel Kamugisha wa S/M  Bukwali akichangia hoja
 Viongozi wa CWT  na wanachama wao,baada ya mkutano walipata' msosi' wa
nguvu na wa viwango


NA MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi Walimu katika kata za Kanyigo na Kashenye wamekitaka Chama Cha Walimu Tanzania(CWT) kurudisha mfumo wa zamani ambapo kata zilikuwa matawi kamili ya chama hicho kuliko ilivyo sasa.
 

Wakiongea jana katika mkutano wao na viongozi wa CWT ngazi ya mkoa na wilaya waliowatembelea,katika mkutano uliofanyika shule ya sekondari Kigarama,walisema mfumo ule ulikuwa wa manufaa makubwa kwao kwani uliwawezesha kukutana mara kwa mara na kujadiliana juu ya utendaji kazi na maslahi yao kuliko ilivyo sasa,na hivyo wameuomba mkutano mkuu wa  CWT Taifa utakaokaa mwezi Novemba kurudisha mfumo huo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kigarama,Samweli Mkella,amekitaka chama hicho kinapotoa semina kwa walimu kukazanie sana wajibu wa mwalimu,badala ya kutanguliza haki za walimu.kwani
maadili ya walimu wa siku hizi hasa vijana yanazidi kuporomoka .

“Usishangae kumkuta mwalimu kijana unamuita ofisini kumsaidia/kumrekebisha juu ya maadili,naye akakuuliza,'mwalimu ulimewahi kupigwa vichwa au ndio nikufundishe?’

 Aidha walimu hao wamesema hawatakuwa tayari kukatwa mishahara yao kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara  za shule za sekondari katika kata zao,kama wanavyosikia tetesi,na badala yake wako tayari kuchangia kama wanavyochangia wanajamii wengine
 

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Kagera,Dauda Bilikesi amewataka walimu wazoefu kuwasaidia walimu vijana ili wawe walimu bora ,badala ya kuwaacha ‘wakifunzwa na ulimwengu’,kwani wakipoteza ajira ni vigumu kurudi kwenye mstari.
Kuhusu kuchangia maendeleo amesema hilo ni suala la kila mmoja ,ila mshahara wa mtu hautakiwi kuguswa na yeyote yule,isipokuwa yale makato yanayotajwa kisheria.

Aidha amewahimiza walimu kutambua wajibu wao kwa mtoto na jamii kwa jumla na wakijua kuwa chama hicho si kichaka cha kuficha maovu ya walimu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau