Bukobawadau

JAMAA AJIKATA KOROMEO !

 Mkazi mmoja wa mkoani Tabora, amejijeruhi vibaya kwa kujikata koromeo akiwa msikitini. Kwa mujibu wa mwandishi Juma Kapipi, mwanaume huyo ambaye jina na chanzo cha kufanya hivyo havijajulikana, amekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora kwa ajili ya matibabu.
Mwandishi huyo alipojaribu kuongea naye, mgonjwa huyo hakuweza kuongea na badala yake aliomba apewe kalamu na karatasi, ambapo aliandika kuwa anaomba atundikiwe damu na kupewa uji kwakuwa ana njaa.
Habari zaidi tembelea>> www.jukwaahuru.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau