Bukobawadau

PICHA UWANJANI KAITABA:KAGERA 1-0 YANGA

 Kikosi Kamili cha timu ya Kagera Sugar kilichoibuka na ushidi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga.
 Kikosi cha timu ya Yanga kilichopokea kichapo na kushuka  hadi nafasi ya  nne ikiwa na point zake 10baada ya kushinda mechi tatu kufungwa mbili na kutoka sare mmoja
 Wachezaji wa Kagera Sugar Wakipiga Jalamba
Wachezaji wa timu ya Yanga Wakiingia Uwanjani.
VIJANA wa kocha Jackson Mayanja Kagera Sugar imeutumia vyema uwanja wake wa Kaitaba baada ya kuifunga Yanga ya Dar es Salaam bao 1-0 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali.
Yanga inayofundishwa na kocha Mbrazili Marcio Maximo jana ilikosa kabisa mbinu za kuipenya ngome ya Kagera Sugar iliyokuwa imedhamiria kupata ushindi kufuati kutoka sare mechi mbili zilizopita kwenye uwanja huo.
 Geilson Santana JAJA,alikuwa wakwanza kufua shuti kali kwenye lango la Kagera lakini lilitoka nje kidogo na kutuliza presha ya mashabiki wa timu hiyo waliokuwa na hamu ya kuona timu yao ikiipunguza kasi ya Yanga.
 Hekaheka langoni mwa Yanga.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa bado hazija fungana na kufanya presha kuwa kubwa kwa mashabiki wa timu zote mbili kuwa juu.
Kagera Sugar walikianza kipindi cha pili kwa kasi na kuliandama lango la mabingwa hao wa zamani Yanga lakini hawakuweza kupata bao katika dakikhizo tatu za awali .
 Mashabiki wa Yanga
Baada ya kuona mambo magumu kocha Jackson Mayanja alimtoa Adam Kingwande na kumuingiza Paul Ngwai na dakika ya 54 mchezaji huyo aliifungia Kagera Sugar bao pekee baada ya kuachia shuti kali lililowapita mabeki wa Yanga na kutinga wavuni.
Taswira sehemu ya mashabiki wakati mtanange ukiendelea
 Wakishangilia bao la Kagera Sugar lililofungwa na Mchezaji Paul Ngwai
'Alhamdulillah rabbil aalameen' anamshukuru Mola Ndugu Mr. Mohamed Hussein ambaye ndiye msemaji wa Kagera Suga
 Wanaonekana wapenzi wa Soka nje ya Uwanja ,Katika Jengo la CCM wakicheck  'Vyabwelele'
 Benchi la Ufundi la Yanga likitafakari
 Kuingia kwa bao hilo kuliionyesha kuizindua Yanga iliyokuwa ikicheza taratibu katika mchezo huo na baada ya kuona mambo magumu kocha Marcio Maximo alimtoa Andrey Coutinho,Haruna Niyonzima na Juma Abduli na nafasi zao kuchukuliwa na Jeryson Tegete ,Hamisi Kiiza na Nizar Khalfani lakini mabadiliko hayo hayakuweza kuwasaidi.
 Ndugu Mwinyi pichabi,mnazi mkubwa wa Kagera Sugar
Ikiwa katika harakati za kusawazisha bao hilo Yanga ilijikuta ikicheza pungufu baada ya Nahodha wake Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moha baada ya kumchezea vibaya Rashid Mandawa wa Kagera Sugar.
Mchezaji  Jeryson Tegete katika utayari wa kuingia Uwanjani
 Andrey Coutinho anafanyiwa mabadiliko nafasi yake inachukuliwa na Jeryson Tegete
Kijana Nabir Juma akifuatilia Soka Uwanjani Kaitaba.
 Hali ya taflani Uwanjani.
Baadhi ya wadau wa Soka wakifuatilia mechi hiyo.
Hicho ni kipigo cha pili kwa kocha Marcio Maximo ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea kwap Brazili baada ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
Lakini pia kipigo hicho kimeifanya Yanga kushuka hadi nafasi ya nne ikiwa na pointi zake 10 baada ya kushinda mechi tatu kufungwa mbili na kutoka sare mmoja.
Jukwaani maneno ya hapa na pale kutoka kwa mashabiki wakati  mpira ukiendelea uwanjani
Bidhaa za Yanga zikionekana kubuma uwanjani Kaitaba
Shabiki wa Yanga akifanya yake.
Mdau Willy Kiroyera Rutta akisalimiana na  Mdau A. Rutayuga,Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF makao makuu.
 Kipa wa Yanga, Juma Kaseja
 Wachezaji wa Yanga wakati wa Mapumziko.
 Kushoto anaonekana Mtangazaji Abdulrazak Majid mtangazaji  88.5 Kasibante Fm.
Kocha wa Yanga Marcio Maximo akiwa  katika benchi kichwa Chini .
Katikati ni Mtangazaji maarufu wa michezo nchini Abdallah Majura akiwajibika
 Kijana Sajidu mnazi wa Kagera Sugar katika hekaheka zake.
 Mashabiki wa Yanga wakitoa machozi katika  mechi hiyo katika uwanja wa Kaitaba
 Usawa wa Jukwaa la Golani.

 Hivi ndivyo Vijana wa kocha Jackson Mayanja wa Kagera Sugar walivyoweza kuutumia vyema uwanja wake wa Nyumbani

 Kijana Obrah Karugila pichani kushoto
 Anaonekana Mwanadada Mdau Salome chui na London.
 Mpaka Mwisho Kagera Sugar 1-0 Yanga
 Kwa matukio zaidi ya picha Ingia katika ukurasa wetu wa facebook kupitia hapa>Bukobawadau Entertainment Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau