Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela
Watu
watatu wamekufa maji akiwamo Padri wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Same,
Amedeus Mangia na wengine tisa kuokolewa baada ya kupigwa na dhoruba
kali wakati wakiogelea kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilayani
Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza
na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu
Ndemanga, alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi na kwamba watu wengine
wawili waliopoteza maisha katika tukio hilo bado hawajatambuliwa majina
yao.
Alisema
walionusurika ni wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Chanjale kinachomilikiwa
na Parokia ya Mtakatifu Stephen ya Same, ambao wote waliokolewa wakiwa
hoi.
Ndemanga
alisema siku ya tukio, wanafunzi hao wakiwa na mwalimu ambaye ni Padri
Amedeus, walikwenda katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kufanya hafla fupi
ya kujipongeza kwa kuogelea na ghafla wakiwa majini, wimbi kubwa la maji
liliwapiga na ndipo baadhi yao wakpoteza maisha.
Watu
walioshuhudia tukio hilo, walisema Padri Amedeus, kabla ya kufikwa na
mauti hayo aliendesha ibada katika kanisa dogo lililopo eneo la bwawani
Nyumba ya Mungu.
Baba mzazi wa padri huyo, Saimon Mangi, alisema mwanaye aliopolewa na wavuvi kutoka bwawani akiwa tayari ameshafariki.
MVUA YALETA MAAFA
Katika
hatua nyingine, Ndemanga ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama katika wilaya yake, alisema kuwa mtoto ambaye bado hajafahamika
jina, mkazi wa kijiji cha Tolowa wilayani hapa, alipoteza maisha baada
ya kusombwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kuonyesha
wilayani humo na maeneo mengine mkoani Kilimanjaro.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela,
alipoulizwa alikiri pia kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
uchunguzi utakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa kwa vyombo vya
habari.
CHANZO: NIPASHE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment