ITV imefika eneo la tukio Kigonsera wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma
na kushudia kijiji cha Kigonsera kikiwa katika hali ya simanzi ambapo
mganga mfawidhi wa kituo cha afya Kigonsera Dkt Patrick Mhagama amesema
wamepokea miili saba na majeruhi ishirini na sita na kwamba miili
imeunngua vibaya kiasi cha kushindwa kutambulika baada ya gari hilo
aina ya Landrover wanten kuwaka moto.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema ajali hiyo ilitokea baada ya
kufeli breki na derva ambaye alikuwa marehemu Padri Hayasinti Kawonga
akakata kona ndipo alipoingia kwenye korongo na ikatokea shoti na gali
likawaka moto huku hilo likiwa ni tukio la tatu katika miaka tofauti
kuua watu saba ambapo kuna wanajeshi saba walikufa kwa ajali ya gari na
kufuatiwa na ajali ya maji ilioyoua watoto saba waliosombwa na maji
katika kata ya Kigonsera.
Mwenyekiti wa kitongoji cha misheni katika kata ya Kigonsera Bw.
John Kafarapia amesema ni pigo kufiwa na padri Kawonga aliyekuwa mkuu wa
shule ya sekondari ya Makatekista na mfadhiri wa wananchi mbalimbali.
CREDIT ITV
0 comment:
Post a Comment