Taarifa zinasema kuwa hali si hali
katika kijiji cha Nyamiyaga Kata ya Bugomora wilayani Kyerwa
vurugu kubwa zinaendelea kati ya watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa
vyama vya CCM NA CHADEMA.
Hali hiyo ya taflani imezukua mida ya
saa 12 jioni ambapo mpaka sasa magari 3 yamevunjwa vioo na
nyumba kadhaa kubomolewa.
Shuhuda wetu anatujuza kuwa tayari amewasiliana na Jeshi la polisi wa kituo kilichopo Mpakani mwa Tanzania na Uganda
Taarifa ya awali inasema vurugu hizo ni kufuatia misafara videdea
vya wagombea kukutana eneo la nyamihanga sokoni Ikiwa mgombea wa
CCM Ndugu Zzawadi Niclous Kazahura alikuwa na mkutano kijiji
cha Nyamiaga alipo maliza mkutano aliondoka na kuwaacha wafuasi
wake wakiendelea kuruka ngoma na muziki "mbele kwa mbele" hapo hapo
eneo husika
Nae mgombea udiwani kupitia Chadema Bw Tulakile
Twijuke Libent Aliyekuwa na mkutano katika kijiji cha Magoma
,mwisho wa mkutano wakitumia barabara moja yenye makutano na eneo la
tukio yalipo makazi halisi ya mgombea huyo hapo ndipo hali ya
sintofahamu ilipo jitokeza .
Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment