Bukobawadau

JUMUIYA YA WANA RUGAMBWA KUKUTANA 23 JAN LEADERS CLUB JIJINI DAR

JUMUIYA YA WANA RUGAMBWA KUKUTANA 23 JAN LEADERS CLUB JIJINI DAR
*Maandalizi ya Jubilee ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Rugambwa ya Bukoba.
Jumuiya ya wana-Rugambwa (Rugambwa Girls Foundation) wanayo furaha kukualika kwenye mkutano wa pamoja utakaofanyika tarehe 23 Januari, 2016 kuanzia saa 7 mchana, Leaders Club jijini Dar es salaam.
Ukiwa kama mdau wa Rugambwa Sekondari: mwanafunzi, mwalimu, mtumishi wa aina yoyote aliyewahi kupita Rugambwa Sekondari pamoja wanafunzi wote waliosoma shule rafiki za Rugambwa (Ihungo, Kahororo, Bukoba Sekondari, Nyakato, Ntungamo Seminari, n.k. tunakualika kushiriki.
Lengo ni kukutana kubadilishana mawazo na kupeana mikakati jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kufanikisha jubilee ya miaka 50 ya Rugambwa Sekondari itakayofanyika, Machi 2016 pamoja na ukarabati na uboreshaji wa shule hiyo.
Atakayesikia au kusoma tangazo hili amfahamishe na mwingine.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Rugambwa Girls Foundation
+255 754 288 671
+255 715 265 158
+255 712 995 991
+255 754 784 545
+255 786 292 402
www.rugambwafoundation.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau