Bukobawadau

TANZANIA KUENDELEZA UTAFITI WA BIOTEKNOLOJIA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Uvuvi, Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa Wema wa siku tatu wa watafiti kutoka nchi za Afrika wa kutathimini utendaji kazi wa Wema kwa mwaka uliopitaKushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Uharishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Dk. Denis Kyetere na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda.
Mkurugenzi wa Ushirikiano Mradi wa Wema, Kampuni ya Monsanto, Mark Edge (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Mkuu wa Programu, Taasisi ya Bill and Melinda Gates Dk.Lawrence Kent (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mradi wa Wema, Shirika la Kimataifa la Uhaurishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Sylvester Oikeh akizungumza katika mkutano huo.
Mtafiti wa Mahindi, Shirika la Kimataifa la utafiti wa ngano na mahindi (CIMMYT), Yoseph Beyene akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mfumo na Uzalishaji wa Mbegu (AATF), Gospel Omanya akitoa mada katika mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Hapa ni kazi tu za utafiti.
Watafiti na washiriki wakiwa Busy na nyaraka.
Watafiti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza utafiti wa bioteknojia pamoja na kutekeleza mradi wa WEMA kwa hatua. Mradi huo unajishughulisha na utafiti wa mbegu za mahindi nchini.

Turuka ameyasema hayo kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi  yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa WEMA, leo asubuhi jijini Dar es salaam. Mkutano huo wasiku tatu umewaleta pamoja watafiti kutoka nchi za Afrika, kutathimini utendaji kazi wa mradi kwa mwaka uliopita.

Alisema awamu ya utafiti wa njia ya kawaida wa mahindi imekamilika na aina  sita mpya za mahindi zimepatikana na kuwa hivi sasa kwa kufuata kanuni za usalama wa viumbe, itaanza utafiti wa mahindi kwa njia ya  uhandisi jeni.

"Sera na kanuni zipo, tutafanya utafiti wa GMO na matokeo ya utafiti yatatoa mwongozo wa dira yetu ya kilimo" alisema Dk. Turuka.

Katika hatua nyingine Dk. Turuka amewataka watafiti wa mbegu za mahindi nchini kuhakikisha mbegu bora walizozifanyia utafiti zinawafikia wakulima kwa wakati.

"Serikali inafurahishwa na mradi huu wa WEMA kwani unamsaidia mkulima kupata mbegu bora ambazo zinahimili ukame na haziwezi kushambuliwa na magonjwa" alisema Dk.Turuka.

Alisema kwa kutumia mbegu bora zilizotokana na utafiti huo mkulima anaweza kupata tani 8.5 za mahindi kwa ekari moja na kusisitiza kuwa mbegu hizo zisipo mfikia mkulima kwa wakati mradi huo utakuwa haujaisaidia serikali.

Dk. Turuka alisema serikali inaangalia kwa karibu sheria na kanuni za kuwapa uwanja mpana watafiti bila ya kuharibu mazingira na kuhatarisha maisha ya wananchi wakati wa kufanya tafiti zao.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda alisema tafiti hizo za mbegu zinatoa nafasi kwa wakulima kupata mbegu bora na kuwa utafiti huo uliofanywa kwa kushirikiana na watafiti kutoka nchi mbalimbali umeonesha mafanikio makubwa.

Mratibu wa mradi huo wa WEMA, Dk.Alois Kullaya alisema mradi huo ulianza mwaka 2008 na kuwa wamekuwa wakitumia mbinu za kisasa kupata mbegu bora.

Alisema Tanzania na nchi nyingine tayari zimepasisha mbegu 59 ambapo kwa hapa nchini zipo mbegu sita tu ambazo zinazalishwa.


Aliongeza kuwa kwa nchi ya Afrika Kusini wao tayari wameidhinisha matumizi ya mbegu za GMO.


Next Post Previous Post
Bukobawadau