Bukobawadau

WANAWAKE WA KYAMURAILE NA RUHUNGA WAHOFIA NDOA ZAO KUVUNJIKA KUTOKANA NA BAA LA NJAA .

Na mwandishi wetu Bukoba.
WANAWAKE katika kata ya Kyamuraile na Luhunga Bukoba vijijini mkoani Kagera wamemulilia mwenyekiti wa halmashauri ya Bukoba vijijini  Murshid Ngeze kutokana na Ndoa zao kuwa katika hatali ya kuvunjika kutokana na baa la njaa kali inayo wakabili.
Kauli hizo zimetolewa na wanawake hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kyamuraile mwenyekiti huyo alipokuwa katika ziara yake ya kutathimini baa la njaa .
Hata hivyo wanawake hao ni pamoja na Agnes Balile Jeralidida Joanseni venansia Domisiani pamoja na sesilia sebasitiani wote wakazi wa kijiji cha Omkalama kata Kyamulaire.
Agnes Balile alisema kuwa kutokana na hali ya njaa inayo wakabili wanaume wa familia wameanzisha tabia ya kuondoka wakidai wanakwenda kutafuta chakula na kutokomea bila ya kurudi hali inayosababisha wanawake kulemewa na familia kutokana na ukosefu wa chakula uliosababishwa na ukame.
Balile alisema kuwa kutokana na ukame uliopo kwasasa hali ya mashamba yaliyokuwa yameandaliwa na kupandwa mazao mbalimbali ikiwa ni Mihogo, Mahindi,Maharage, na Migomba imekauka kiasi kwamba watu wamefikia wakati wa kula mlo mmoja kwa siku na hata wakati mwingine  watu wanalala njaa hata siku mbili.
"Nikuombe mwenyekiti wetu wa halimashauri Ngeze fikisha vilio vyetu kwa serikali watu tuna kufa njaa hatujui hatima yetu na watoto wetu fikilia mimi nina watoto watano na wajukuu zangu watatu nahangaika jamani hata unga wa uji unakosa tusaidieni jamani waume zetu wametukimbia na watoto wetu watanza kutukimbia"alisema Balile
Jeralidida Joanseni alisema kuwa kutokana na hali ya ukame uliopo wanawake wanakumbwa na changamoto mbalimbali ambapo inafikia mama anaamua kuanzisha mahusiano na mwanaume yeyote ili aweze kupata chakula kutokana na mashamba yao kukauka kwa na ukame kabisa.

Joanseni alisema kuwa njaa ina sababisha mambo mengi sana ambayo athali zake zinaweza kutokea kwasasa au badae ambopo yanaweza kulipuka magonjwa na kuongeza wahalifu kataka jamii kutokana na baa la njaa.
"Nina amini kuwa hakuna alielileta baa la njaa na sio serikali au mtu yeyote bali ni mitihani ya mungu hivyo Serikali kuanzia ngazi ya kijiji wanatakiwa kusaidia maana hali inazidi kuwa ngumu siku hadi siku kutokana na njaa kali inayo tukabili"alisema Joanseni
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Bukoba vijijini Murshid Ngeze aliwaereza wananchi hao kuwa swala la njaa lisichanganywe na siasa huu ni wakati wa kutulia na kujituma katika kazi na kuuomba pasipo kukoma.
Ngeze alisema kuwa katika baa hili la njaa viongozi wa vijiji na wa kata wasiutumie matatizo ya wananchi kuwa miladi yao ya kujinufaisha katika maisha yao na atakae gundulika anafanya hivyo atawajibishwa kisheria.

"Niwatake akina mama kutulia katika familia zenu na kuiona hii kama changamoto ambayo ni yamuda mfupi tu na inapita, na mimi ninakwenda kufikisha tarifa hizi kwa kamati ya maafa ili tuone jinsi ya kusaidia katika hali hii"alisema Ngeze
Pia wananchi niwaombe kujenga tabia ya kutunza vyakula vya akiba katika familia zetu ili inapotokea hali kama hii ya ukame na njaa vyakula hivyo viweze kutusaidia.
MWISHO.
Next Post Previous Post
Bukobawadau