Bukobawadau

TAMASHA LA KUFANYA MAZOEZI NA KUPIMA AFYA KUFANYIKA JUMAMOSI DAR

Msemaji wa chama cha Maafisa Mawasilino Serikalini (TAGCO) Bw. Abel Ngapemba  (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la  kufanya mazoezi, kupima afya,kuchangia damu,leo jijini Dar es Salaam katika  ulioshirikisha Jukwaa la Wahariri (TEF) pamoja na Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam. Tamasha hilo litafanyika siku ya Jumamosi  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  Kuotoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Theophil Makunga na Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Siyovera Hussein.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa (wa kwanza kulia) akitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Tamasha la Mazoezi ambalo litawapa wananchi fursa ya kufanya mazoezi  na kupima afya bure kuitikia wito wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.Wengine ni wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo.
Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Siyovera Hussein akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)  leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliolenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika Tamasha linalolenga kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi . Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Theophil Makunga.


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo Leo Jijini Dar es Salaam.
 (Picha na: Frank Mvungi - Maelezo)
Next Post Previous Post
Bukobawadau